Mwanamke mkongwe zaidi nchini Marekani mmoja wa watu wachache waliozaliwa katika karne ya 19, amefikisha miaka 115.
Jeralean Talley alizaliwa tarehe 23 mwezi Mei
mwaka 1899 na ni mtu wa pili mkongwe zaidi duniani kwa mujibu wa shirika
moja la utafiti la Marekani la GerontologyAnajiandaa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na familia yake na marafiki kanisani mjini Michigan siku ya Jumapili.
Alizaliwa katika jimbo la Georgia, na kuhamia Michigan mnamo mwaka 1935 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mumewe ambaye alifariki mwaka 1988.
Bintiye kwa jina Thelma Holloway, ana umiri wa miaka 76.
Bi Holloway humchunga mamake na ingawa aliwahi kushiriki shughuli ya uvuvi ishara kuwa afya yake ni nzuri yeye hutembea kwa usaidizi.
Endelea kutembelea katemimethsela.blohspot.com uweze kujua mambo mbalimbali ambayo si rahisi kuyajua kupitia sehemu nyingine
0 comments:
Post a Comment