BEKI mfaransa, Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United , klabu imethibitisha.
Evra alitazamiwa kuondoka baada ya United kuweka ofa ya paundi milioni 27 kwa beki wa kushoto wa Southampton , Luke Shaw.
Lakini beki huyo ameamua kubakia kwa mwaka mmoja katika ubosi wa kocha mpya Louis van Gall.
Anabaki: Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United.
Mapema
wiki hii, Evra aliripotiwa kuwa na mazungumzo na Juventus, lakini sasa
atapambana na Shaw katika namba yake endapo tu Man United itafanikiwa
kumsajili beki huyo wa kimataifa ya Uingereza majira ya kiangazi mwaka
huu.
Kitendo
cha Evra kuongeza mkataba kitapokelewa kwa furaha na mashabiki wengi wa
Man United ambao wana mapenzi ya moyoni na beki huyo mwenye miaka 33
tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2006 akitoka Monaco.
Evra pia ni mchezaji anayependwa na wenzake katika vyumba vya kubadilishia nguo, pia anasifiwa kwa uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Beki
huyo wa zamani wa Nice, aliyeichezea United mechi 379 alionesha kiwango
kizuri msimu uliopita, licha ya klabu kudoda katika kipindi hicho cha
David Moyes.
Aliifungia
United bao la kuongoza katika mchezo wa robo fainali ya UEFA dhidi ya
Bayern Munich, japokuwa haikutosha kuwabakisha kwenye mashindano katika
uwanja wa Allianz Arena.
Evra
(kulia) kwasasa yupo katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa
kujiandaa na fainali za kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil
0 comments:
Post a Comment