Mfumo wa jiji la Dar Es Salaam uko kwenye mchakato wa kubadilika.
Hayo
yamesemwa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala kwenye mkutano wa
Global Lab on Metropolitan Strategic Planning unaofanyika jijini Seoul,
Korea Kusini.
Akiwasilisha mada ya jinsi mfumo wa
uendeshaji majiji unavyochangia utoaji huduma, Meya Silaa ameeleza
matatizo ya mfumo usio na muingiliano wa jiji la Dar es Salaam na
Manispaa zake na mamlaka nyingine nyingi zinazohudumu kwenye jiji la Dar
es Salaam zikiwemo Sumatra, Ewura, Dart, Tanesco, Dawasa, Dawasco,
Tanroad, Tamesa na mamlaka nyingine bila kuwa na mfumo wa usimamizi wa
kiutendaji.
Meya Silaa ameeleza kuwa katika mradi wa DMDP
unaogharamiwa na Benki ya Dunia umefanyika utafiti wa namna ya mfumo wa
jiji la Dar Es salaam yaani Institutional Review Analysis (IRA) na
Development of Institution Strengthening Plan(ISPs) kwa kila manispaa na
kuwa na mfumo bora wa jiji la Dar Es salaam.
Dar Es Salaam ndio mji mkubwa Tanzania
unaobeba majukumu karibu yote ya kiserikali na kibiashara ukiwa na
Bandari ya Dar es salaam na wakaazi milioni 4.4 sawa na asilimia 10 ya
wakazi wote Tanzania na ukuaji wa asilimia 5.6 na kuwa jiji la tatu
Afrika na la tisa duniani kwa ukuaji.
Kufikia 2025 jiji la Dar Es Salaam
linakadiriwa kuwa na wakaazi milioni 8.9 na wakaazi milioni 15.3 kufikia
mwaka 2035 na hivyo kuingia kwenye orodha ya majiji makubwa “World Mega
Cities List”.
Ni wakati sasa wa kuiangalia Dar Es Salaam kwa umakini mahususi
0 comments:
Post a Comment