Baadhi ya madereva wanachama wa Chama cha Madereva wa
Serikali Tanzania (CMST), wameilalamikia serikali kuendelea kuwalipa
ujira mdogo huku wakidai kwamba serikali imeajiri madereva wengi
kwa kutumia sheria ya mkoloni ijulikanayo kwa jina la Operation
Service ambayo kwa kiasi kikubwa inawakandamiza madereva
kimaslahi.
Wakizungumza katika kikao cha viongozi wa madereva wa chama hicho
mkoa wa Ruvuma kilichofanyika mjini Songea, madereva hao
wamesema chama hicho chenye wanachama zaidi ya 900 hapa nchini,
kilianzishwa kwa lengo la kupingana na sheria za mkoloni
zinazomnyima dereva kupata haki zake za msingi lakini bado
madereva walio wengi licha ya kudharaulika na waajiri wao lakini pia
wanaendelea kulipwa ujira kiduchu.
Pamoja na hatari mbalimbali zinazowakumba madereva hao katika
kazi zao, ikiwemo mwendo wa kasi katika misafara ya viongozi
wakubwa wa kitaifa, wanawapigia magoti waajiri wao kuwaomba
angalau kuwafikiria upya mishahara yao ili waweze kumudu gharama
za maisha ambazo zinazidi kuongezeka siku hadi siku.
0 comments:
Post a Comment