Facebook

Friday 2 May 2014

Shabiki aliyemrushia ndizi Dani Alves akamatwa Hispania....................

dani alves 

Polisi wa Hispania wamesema wamemkamata mshabiki anayeshukiwa kumrushia ndizi mchezaji wa Barcelona, Mbrazili Dani Alves wikiendi iliyopita.
Kitendo hiko cha kibaguzi kilifanyika wakati mchezaji huyo alipokuwa kwenye kona ya uwanja kwenye mechi ya Villareal siku ya Jumapili iliyopita.
Alves alijibu kwa kutoa maganda na kuila ndizi hiyo, kitendo ambacho kilisifiwa ulimwenguni kote na kuibua kampeni kubwa mtandaoni inayopinga ubaguzi wa rangi.
Mtu huyo aliyeshikiliwa ana umri wa miaka 26 na ni shabiki wa Villareal.
Shabiki huyo anajulikana kwa jina la David Campaya Lleo, kilisema chombo cha habari cha hapo.

Klabu ya Villareal imesema mapema kuwa mtu huyo alikuwa na tiketi ya msimu mzima ambayo imefutwa na amefungiwa maisha kuingia uwanjani.

0 comments:

Post a Comment