Facebook

Tuesday 6 May 2014

Karibu ACT-TANZANIA, wewe ndio mbadala wa CHADEMA na CCM


Chama kilichovunja rekodi kwa kupata usajili wa kudumu miezi michache mara baada ya usajili wa muda; ACT-TANZANIA leo ndio kimekabidhiwa cheti chake cha usajili wa kudumu rasmi na masajili wa vyama vya siasa mara baada ya kumalizika zoezi la usajili lililofanyika katika
mikoa kumi iliyoteuliwa
 
kilifanikiwa kumaliza zoezi la uhakiki mara baada ya kuruka vihunzi vingi toka kwa wahafidhina na watu wasiopenda siasa za ushindani. Katika zoezi letu tumekumbana na vikwazo vingi ikiwa pamoja na uchomekaji wa wanachama fake waliotumwa kwaajili ya kazi ya kujifanya wako tayari kuhakikiwa lakini kwa lengo la kutojitokeza siku ya kuhakikiwa, jambo ambalo wahafidhina na maadui zetu walikuwa hawajui ni kuwa chama chetu kinapendwa na wananchi hivyo wengi walijitokeza kiasi cha kuziba mapengo ya mamluki ambao kwa makusudi hawajajitokeza siku ya kuhakikiwa. Pamoja na hayo tunatambua wanachama wetu waaminifu waliotaka kujitokeza lakini sababu zilizo nje ya uwezo wao zilipelekea washindwe kujitokeza siku ya kuhakikiwa.

0 comments:

Post a Comment