Friday, 22 May 2015
Jinsi ya kutengeneza blog kwa kutumia Google Blogger
Blog ni nini ? Blog inasimama badala ya Web-Blog na inatumika kwajili ya kushare vitu kama knowledge, opinion, photos, music, event, poetry/poem, na vitu vingine.
Je Blogger ni nini? www.blogger.com inajulikana kama Blogger na ni tool ama website amabayo unaweza kutengeneza blog nzuri bure.
Hapo nyuma, kutengeneza blog ilikua ni kazi ngumu kwa sababu ilitakiwa ujue baadhi ya web languages kama: CSS, HTML ama PHP. Ila sasa unaweza kutengeneza blog bila kujua Languages hizi kabisa kwa msaada wa WYSIWYG interface. Ila kujua languages hizi itakusaidia kuwa na ubunifu zaidi kwenye blog yako.
Blogger ni moja ya best free blogging platform kwajili ya kutengeneza blog. Kufanya Setting ya blog kwa kutumia Blogger ama Blogspot blogging platform inaweza kufanyika kwa dakika 10. Ila kabla ya kuanza maisha yako kama blogger, Kuna vitu unatakiwa kuvijua.
1. Aina ya blog yako– Kuna aina tatu kuu za blog:
Personal Blog
Collaborative Blog- inahusisha zaidi ya mwandishi mmoja
Topical Blog- inajihusisha na aina moja ya somo
2. Hakikisha blog unayotaka kutengeneza ina maana na inahusisha wasomaji wako
3. Unatakiwa kuwa na uamuzi ni jinsi gani unakuwa unapostt kwenye blog yako.
4. Kabla ya kutengeneza blog yako, hakikisha una vitu kama vitano ambavyo utavipost kuzuia kuwa na empty blog.
5. Inatakiwa uwe na wazo la jinsi unavyotaka blog yako ionekane kama vile rangi na design yake .
Hatua za kutengeneza Blog kwa kutumia Blogger Service
Hatua ya 1. Unatakiwa kuwa na Google Account (Gmail Account). Unaweza kuipata hapa www.gmail.com
Hatua ya 2. Baada ya kuwa na gmail account inayofanya kazi, endelea na usajili wa blog kwenye www.blogger.com kwa kuclick sign up button iliyopo kwenye top right corner.
Hatua ya 3. Kisha, jaza fomu kwa taarifa sahii na zinazohitajika na kisha click continue button.
Hatua ya 4. Hapa utatakiwa kujaza jina la blog yako " Blog Title " na "URL" katika nafasi husika. Sasa unatakiwa kuchagua jina la blog yako kutokana na vile unavyopenda kisha click continue.
Hatua ya 5. Unachotakiwa kufanya hapa ni kuchagua template kwenye Blogger templates library (unaweza kubadilisha templates hii muda wowote ).
Hatua ya 6. Sasa blog yako iko tayari, na unatakiwa kuanza kupost. Kupost kwenye blogger blog platform ni rahisi hata mtu mwenye uwezo mdogo wa kujua computer anaweza kufanya.
Hatua ya 7. Sasa unatakiwa kuifanya blog yako iwe inaonekana zaidi , unique na professional kwa kuwa na domain name kwajili ya blog yako.
Hatua ya 8. kwa maswali na tips zaidi, unaweza kutembelea Blogger helpful site.
Kama umekutana na tatizo lolote katika kufungua blog yako , check www.bantutz.com kwa msaada
0 comments:
Post a Comment