Facebook

Monday, 1 June 2015

Wanaharakati walishutumu jeshi la Iraq

Wanaharakati wa haki za binadamu wanalishutumu Jeshi la Iraq kwa kushindwa kuokoa maelfu ya watu kufikia sehemu salama ya nchi hiyo mara baada ya wao kukimbia mapigano katika jimbo la Anbar .
Wanaharakati hao wanasema serikali - ambayo inawaongoza ina waslamu wengi wa madhehebu ya Shia inawabagua Waisalamu wa madhehebu ya Suni waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Islamic State aambao nao pia ni Waislamu wa Suni.
Kwa wale wanaojaribu kuingia Baghdad wanakutana na vikazo vya barabarani katika mitaa ya mji ambapo hatua za kiusalama kwa ajili ya ulinzi zinachukuliwa.
Familia za Sunni zimekutwa zikiwa zimekwama eneo hilo zikiwa na hali mbaya ambapo wanafikiria kurejea kwenye maeneo yaliyoshikiliwa na IS.

0 comments:

Post a Comment