Facebook

Thursday 8 May 2014

Pombe yenye sumu yawaua 70 Kenya



Washukiwa waliouza pombe hiyo wameripotiwa kukamatwa
Watu wawili wamekamatwa nchini Kenya kuhusiana na mkasa wa watu 70 kufariki kutokana na kunywa pombe iliyokuwa imetiwa sumu.
Vifo hivyo vimetokea katika muda wa saa 48 baada ya walevi kuanza kulewa siku ya Jumapili na Jumatatu asubuhi.
Pombe hiyo iliyopewa jina la 'Countryman', inasemekana iliwekwa sumu aina ya Methanol na kusababisha baadhi ya waliokuwa wamekwenda kuibugia kufariki huku wengine wakisalia hali mahututi na wengine kupoteza uwezo wao wa kuona.
Madaktari wanafanya kila wawezalo kujaribu kuokoa baadhi ya waathiriwa ambao wamelazwa hospitalini.
Vifo hivyo vilianza kutokea mapema wiki hii katika mkoa wa kati na katika eneo la Mashariki mwa Kenya.
Inaarifiwa wengine wengi wamelazwa hospitalini baada ya kubugia pombe hiyo.
Idadi ya vifo ilianza kuongezeka huku watu wengine 14 wakifariki katika jimbo la Embu Mashariki mwa nchi , wengine wanne wakifariki katika jimbo la Makueni. Watu 75 wamelazwa hospitalini katika jimbo hilo wengine watatu wakiripotiwa kupoteza uwezo wao wa kuona.
Kwa sasa wataalamu wanafanyia utafiti kinywaji hicho pamoja na mkojo kutoka kwa wagonjwa kubaini kilichowekwa ndani ya pombe hiyo.
Matokeo yanatarajiwa katika siku mbili zijazo.

0 comments:

Post a Comment