Manchester City imepiga hatua
muhimu katika kuwania taji la ubingwa wa ligi kuu ya England wakirejea
kileleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya magoli na Liverpool baada ya
kuibwaga Everton, Jumamosi 3-2.
Liverpool katika mchezo wa jana ilikuwa
inawaombea majirani zao Everton kuwabwaga Manchester City, na matumaini
ya kufanya hivyo yalipanda baada ya Ross Barkley kuifungia Everton bao
la mapema dakika ya 11.Everton hawakukubali kuchinjwa kikatili katika uwanja wao wa nyumbani. Romelu Lukaku akafunga goli la pili katika dakika ya 65.
Everton waliendelea kushambulia kutafuta angalau pointi moja, lakini Manchester City wakipigana kutoka na pointi zote tatu. Na ikwa hivyo hadi kipenga cha mwisho Manchester City waliibuka na ushindi wa magoli 3-2.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo, Manchester United nayo imezidi kupatwa na masahibu baada ya kukung'utwa na Sunderland 1-0 katika mchezo wao wa Jumamosi na hivyo kurejea katika nafasi yake pendwa ya 7 msimu huu wakiwa na pointi 60 na hivyo kuwa na uhakika wa kukosa ubingwa wa ligi kuu ya England na pia mashindano ya UEFA msimu ujao.
Fulham na Cardiff tayari zimeshuka daraja, hivyo msimu ujao hazitakuwa tena miongoni mwa timu 20 za ligi kuu ya England. Fulham mpaka inaporomoka ilikuwa imejikusanyia pointi 31, huku Cardiff ikiambulia pointi 30 tu.
Sunderland na Norwich zinakabana ili kujinasua na balaa la kushuka daraja na kuungana na Fulham na Cardiff. Sunderland ina pointi 35 na Norwich ina pointi 32.
0 comments:
Post a Comment