Facebook

Tuesday 6 May 2014

Uchunguzi kumbe Makalio Makubwa Kuna Vingi Ndani Yake


Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.

Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari.


Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.

Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.

Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari. Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka.


Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.

0 comments:

Post a Comment