Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG imeamplfy kwamba kitendo
cha Serikali kukosa nyaraka za mali zake kumechangia baadhi ya
watendaji wasio waaminifu kutumia mwanya huo kujisogezea mali za umma.
Katika ripoti yake ya Ukaguzi kwa mwaka 2013 CAG Ludovick Utouh amesema
ofisi yake imebaini upotevu wa magari 11 yaliyonunuliwa kwa ajili ya
matumizi na mamlaka ya maendeleo na biashara Tanzania (TanTrade) ambayo
hadi sasa hayafahamiki yalipo.
Ofisi yake inalifanyia uchunguzi suala hilo na tayari imegundua hayo
magari yalisajiliwa kwa namba binafsi badala ya namba za serikali huku
akisema ‘wizara ya viwanda na biashara ilinunua magari kwa ajili ya bodi
ya biashara na tunaomba kusema magari hayo tumejaribu kuyafatilia
lakini hayaonekani na hayajulikani yalipo na ni magari mapya
yalinunuliwa kwa ajili ya TanTrade lakini TanTrade wenyewe wanasema
hawajayapokea na Wizara inasema haijui yako wapi’
0 comments:
Post a Comment