Ugonjwa wa homa ya dengue ambao umezidi kusambaa mkoani Dar es Salaam na kuathiri wilaya zake tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni umezua hofu na taharuki kubwa kwa wananchi. Takwimu za Kitengo cha Utafiti wa Magonjwa cha Ifakara (IHI), kimeweka kambi katika Hospitali ya Mwananyamala hapa jijini kutafiti aina za homa zinaonyesha kuwa, kwa miezi miwili ya Machi na Aprili pekee, wagonjwa 85 walibainika kuwa na ugonjwa huo
Sisi tunadhani Serikali inastahili lawama kwa kutochukua hatua stahiki
mapema kupambana na ugonjwa huo, ambao uliingia Dar es Salaam kwa mara
ya kwanza mwaka 2010 na kuua wanafunzi kadhaa wa Chuo cha Usimamizi wa
Fedha (IFM). Juni mwaka jana, Wizara ya Afya ilithibitisha kuwapo kwa
ugonjwa huo na Machi 26 mwaka huu, ilitoa taarifa kwa umma, ikisema
wagonjwa 70 walikuwa wamebainika, 58 kati yao wakiwa Kinondoni, saba
Temeke na watano Ilala.
Hata hivyo, wizara hiyo haikupaswa kuishia katika kutoa taarifa tu
pasipo kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi nchi nzima kuhusu ugonjwa
huo, namna ya kujikinga na nini cha kufanya iwapo wataambukizwa.
Ulihitajika uwazi badala ya usiri, vinginevyo ugonjwa huo usingeenea kwa
kasi tunayoishuhudia hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment