Facebook

Thursday, 1 May 2014

Unakijua alichokisema Diego Costa kuhusu kujiunga Chelsea...fuatilia hapà


MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa, ameitandika Chelsea bila huruma na kuisaidia klabu yake kufuzu fainali licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa atajiunga na Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu.
Costa alifunga bao la penati na katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea na kumfanya Diego Simeone akutane na Carlo Ancelotti katika mchezo wa fainali mjini Lisbon nchini Ureno mwezi ujao.
Mtandao huu kupita mtandao rafiki wa Goal.com unafahamu kuwa Chelsea wametenga kitita cha pauni milioni 35 kukamilisha usajili wa nyota huyo mwenye miaka 25.
Costa amekiri kuwa kwasasa hajaamua maisha yake ya baadaye.
“Kucheza Chelsea baadaye? Tutaona, najua kuna ofa kwa ajili yangu, najisikia vizuri kuwepo Atletico” ameuambia mtandao wa Sky Italy.
Adrian Lopez na Arda Turan pia walifunga, lakini Chelsea walikuwa wa kwanza kufumania nyavu za Atletico kupitia Fernando Torres.
Costa ameuelezea mchezo wa leo kuwa ni “wa maajabu na historia” na amemsifu kocha wake Diego Simeone kuifanya Atletico kuwa na makali zaidi msimu huu.
“Ni kitu cha ajabu na kihistoria. Tumejituma kwa nguvu zote kufika fainali hii”. Costa amezungumza na Canal Plus.
“Mpira haukuishia kwenye penati tu, lakini ulimalizika vizuri. Nadhani timu inafanya vitu sahihi, lakini Diego Simeone amefanikiwa kufanya maamuzi sahihi kila wakati”.

Related Posts:

  • Wadhamini wa kombe la Dunia taabani. Hadhi ya makampuni yanayothamini kombe la Dunia taabani Brazil. Udhamini wa kandanda duniani umekua kwa kiasi kikubwa na sasa unazidi utoaji wa fedha kwa mashirika yanayoisimamia kwa shirika la soka duniani Fifa.Ki… Read More
  • Maajabu ya mmiliki wa klabu ya Southampton.. Katharina Liebherr: Jina hili la mama huyu kibonge si maarafu sana katika vichwa na midomo ya wapenda soka duniani hasa bongo,labda ni kwa sababu ya jinsia yake ama ni kutokana na tabia yake ya kujiweka mbali na vyomb… Read More
  • Ulaya wataka Blatter ajiuzulu kwa usemi Rais wa Shirikisho la kandanda duniani, FIFA, Sepp Blatter. Maafisa wa kandanda wa Europa sasa wamemtaka rais wa shirikisho la kimataifa… Read More
  • Brazil 3-1 Croatia 00:55 Mechi imekamilika . Brazil 3-1 Croatia . 00:54 Mechi hii imekamilika Brazil ikisajili ushindi mkubwa wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia. … Read More
  • Matumaini ya Brazil yako kwa Neymar Pele; Neymar asiachiwe mzigo pekee yake Mchezaji wa kitambo wa Brazil ana wasiwasi kuwa taifa hilo linamshinikiza mshambulizi wa Neymar kuisaidia taifa hilo kunyakua taji la Kombe la Dunia kwa wenyeji hao na huen… Read More

0 comments:

Post a Comment