Aki akiwa na mke wake.
Msanii
wa filamu za Kibongo, Meya Shaban ‘Aki wa Bongo Muvi’ ameachana na
ukapera baada ya kufunga ndoa na msanii mwenzake, Amina Shaban, Ijumaa
Wikienda lilikuwepo ndani ya nyumba.
Staa
huyo wa Sinema ya Devil Kingdom ya mwigizaji Emmanuel Myamba ‘Pastor
Myamba’ alifunga ndoa hiyo Ijumaa iliyopita kwenye Msikiti wa Mbezi,
Tanki-Bovu, Dar na kufuatiwa na bonge la sherehe katika Ukumbi wa Mbezi
Beach Park.
Katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari wetu, ilipambwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa filamu za Kibongo.
Shughuli
hiyo ya kukata na shoka iliwashangaza watu kutokana na maharusi hao
majina ya baba zao kufanana huku wageni waalikwa wakisema kwamba
ikitokea hivyo ndoa huwa inadumu kwa muda mrefu.
Akizungumza
mbele ya wageni waalikwa, Aki wa Bongo Muvi alisema kuwa anamshukuru
Mungu kwa kuwa ametimiza ahadi ya ndoa kwani mara ya kwanza walikutana
na mkewe kwenye Chuo cha TFTC cha Pastor Muyamba na kuanzisha urafiki
hadi wakafikia hatua hiyo ya ndoa.
“Namshukuru
sana Pastor Muyamba kwani ndiye mwalimu wangu wa sanaa na kama siyo
sanaa, nisingempata mwanamke kama huyu, yaani siku ya leo nina furaha
sana,” alisema Aki wa Bongo Muvi ambaye ameandika historia kwa tukio
hilo.
Baadhi
ya wasanii waliohudhuria kwenye sherehe hiyo ni Pastor Muyamba, Zawadi,
Nova ambaye alikuwa mshehereshaji na Rais wa Shirikisho la Filamu la
Tanzani (TAFF), Saimon Mwakifwamba ambaye aliwapongeza kwa hatua hiyo ya
kuingia kwenye ndoa huku akiwataka wasanii wengine kuiga mfano wao.
Baadhi
ya sinema alizoigiza Aki wa Bongo Muvi aliyezidiwa urefu kiaina na
mkewe ni pamoja na The Lost Sons, Sometime Yes, Sometime No, Yes Madam,
Devil Kingdom, Pastor Muyamba Temptation, Uncle Mpozemenye na nyingine.
0 comments:
Post a Comment