Facebook

Friday 9 May 2014

Je unayajua masharti magumu walioyatoa upinzani ili kushiriki uchaguzi mkuu 2015 ?.....




Serikali imetakiwa kuandaa taratibu za mpito za kushughulikia Uchaguzi Mkuu ujao ili kunusuru nchi kuingia katika mtanziko unaoweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa, endapo utafanyika bila kupatikana kwa Katiba Mpya la sivyo Kambi Rasmi ya haitashiriki.
 
Hayo yalielezwa jana na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa hotuba ya kambi hiyo bungeni kuhusu Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Hatuwezi kuingia uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa kwa utaratibu uliopo leo, hatuwezi kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani na Tume ya Uchaguzi kama ilivyo leo, hatuwezi tena kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani wakati matokeo ya uchaguzi wa Rais hayawezi kuhojiwa mahakamani.”


Aliongeza: “Hatuwezi kuingia kabla na hoja ya mgombea huru haijapatiwa majibu, tukiwa na daftari la wapigakura lililopo leo na hatuwezi kulikubali daftari jipya litakalotengenezwa kama wadau wote hatutashirikishwa kikamilifu.”


Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwasilisha bungeni, Bajeti ya ofisi yake ambayo imetenga Sh5 bilioni kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.


Mbowe alisema kama ilivyo kawaida, Serikali na CCM inaweza kupuuza tahadhari hizo na kulazimisha kwenda katika chaguzi hizo katika mazingira ambayo hayana mwafaka kama inavyoonekana sasa katika Mchakato wa Katiba Mpya.

0 comments:

Post a Comment