Facebook

Monday, 5 May 2014

Taarifa kamili kuhusiana na milipuko minne iliyotokea Kenya wiki iliyopita.....

TZA KUTOA CHA MA BASI YA CHANIA MOMBASA 
Baada ya kutoka kwa video kwenye mtandao wa alkataib wanamgambo wa kigaidi wa alshabaab watekeleza ugaidi nchini Kenya na kuwaua watu watano katika miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya.
Mei 3 majira ya saa 2 usiku milipuko miwili yalitokea kwa mpigo Mjini Mombasa moja katika eneo la Nyali hoteli ya Reef iliyomuua mtu mmoja na nyingine eneo la kituo cha mabasi cha Mwembe tayari .
Mashuhuda wa  tukio hilo wamesema kwamba mtu aliye kua katika gari aina ya Toyota Probox Alirusha bomu kuwalenga wasafiri walio kua wakisubiri kufika kwa basi.
Bomu hilo lililokua ndani ya mkoba kilicho kua kimetelekezwa ufuoni mkabala na hoteli ya reef kililipuka katika eneo la lango lilipokua likikaguliwa na walinzi baada ya mtu mmoja kukiona na kukisalimisha kwa walinzi akidhani mwenyewe amekisahau.
Jumapili Mei 4  jiji la Nairobi watu 3 waliaga dunia na wengine 60 walijeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili  kwenye mabasi mawaili tofauti katika barabara ya Thika super Highway jijini humo,mlipukohuo unasemekana ulitokana na vilipuzi vya IEDS vilivyokua vimewekwa katika mabasi hayo yaliyo kua yakiwasafirisha watu kutoka katikati mwa Jiji.
TZA BASI BAADA YA MLIPUKO NAROBI 
Taarifa kutoka maafisa wakuu wa polisi na mashuhuda wa matukio hayo wamesema kwamba mlipuko wa kwanza ulitokea saa 11 jioni karibu na eneo la homeland ambapo basi la Jeean Sacco lililipuka likiwa linaeleka Githurai 45,tukio la pili lilitokea dakika kadhaa baadaye katika mzunguko wa Roysambu katika basi la Mwi sacco lilokua na abiria 51 waliokua wakisafiri kwenda mwiki.
Hadi sasa wameripotiwa kufariki kwa watu 6 kufuatia shambulizi dhidi ya mabasi mawili jijini Nairobi na wanne Mombasa,baada ya shambulizi  kwenye kituo cha mabasi mwembe tayari na katika hoteli ya Reef kule Nyali.
Kenya imekabiliwa na zaidi ya mashambulizi 80 na watu 300 wamefariki tangu wanajeshi wa Kenya kuanza kuwakabili wanamgambo wa Alshabaab kule Somalia.

Endelea kyembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri nchini Kenya

Related Posts:

  • Obama aahidi kushirikiana na Republican   Kiongozi mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani. Wanachama wa Republican wa… Read More
  • Wakazi waahidiwa dola mia kwa kukamata mbu Taiwan.   Wakazi katika mji mmoja nchini Taiwan wameahidiwa zawadi nono kwa kukamata mbu. Shindano hilo lilitangazwa na idara ya afya ya jiji la Kaohsiung, linalenga kupambana na mlipuko wa mbu wanaosababisha homa ya d… Read More
  • Meya anayetuhumiwa kuua akamatwa Mexico   Polisi nchini Mexico wamemkamata meya wa mji wa Iguala, pamoja na mke wake ambako wanafunzi 43 walipotea mwezi Septemba.   Jose Luis Abarca ambaye amekuwa akitafutwa amekamatwa na maafisa wa polisi katika mji … Read More
  • Je,wajua kuna waombolezaji wa kulipwa ?   Kila Alhamisi na Ijumaa, shughuli katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, huvurugika kwa sababu mamia ya waendesha pikipiki huzuia barabara kutokana na kukodiwa kuomboleza msiba kwa malipo. Kelele za saut… Read More
  • Wanajeshi wa Libya wafukuzwa Uingereza.   Wanajeshi kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi. Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni n… Read More

0 comments:

Post a Comment