Facebook

Thursday, 22 May 2014

Umeiskia hii kuhusu Loliondo,,sasa hivi sio kikombe cha babu ni Dhahabu.



dha Inasemekana kuwa kwa sasa kuna watu wengi wanaenda Samunge,Loliondo na kinachowapeleka huko si  Kikombe cha babu tena sasa hivi ni madini ya dhahabu ambayo inasemekana yamegundulika eneo hilo.

Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa watu wanaongezeka kijijini hapo kwa ajili ya kujipatia madini hayo yanayosemekana yapo katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na kwa Babu.

Diwani wa Samunge Jackson Sandea amesema kwa sasa kuna zaidi ya watu 4,000 na bado wanaongezeka na kusema kuwa idadi hiyo ya watu inaweza kuwa zaidi ya kikombe cha babu kwa kipindi kile.
Ingawa eneo rasmi zaidi bado halijatjwa ila inasemakana mbali na kupatikana kwenye mto huo pia dhahabu hiyo ianapatikana hata kwenye mashamba ya watu,kwa sasa Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini Alex Magayane amesema wanajiandaa kwenda kijijini hapo baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu kwenye eneo la Samunge.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri kuhusiana na maajabu yanayoendelea kutokea huko Samunge,Loliondo.

0 comments:

Post a Comment