Mchezaji gofu nambari kumi
duniani Rory McIlroy amevunjilia mbali mipango ya harusi yake na
aliyekuwa mchezaji tenis nambari moja duniani Caroline Wozniacki.
Raiya huyo wa Ireland ambaye ni bingwa wa mataji
mawili ya gofu duniani amewaambia waandishi wa habari kuwa aligutushwa
na kadi za mwaliko wa harusi yake na akang'mua kuwa hayuko tayari kwa
majukumu ya ndoaMcIlroy alisema hakuna njia bora ya kuvunja uhusiano baina ya wachumba lakini mimi ninamtakia kheri Wozniacki katika maazimio yake ya baadaye.
McIlroy ambaye anajiandaa kwa mchuano wa 'The BMW PGA Wentworth utakaoanza hapo kesho nchini Uingereza ,amesema kuwa atajitahidi kumakinikia mchuano huu kwani sasa mambo ya uchumba yamepita.
Wozniacki, kwa upande wake anajiandaa kwa mchuano wa tenis ya wazi ya Ufaransa utakaonza tarehe 25 mwezi huu .
Wachanganuzi wa maswala ya mahusiano baina ya wachezaji wenye ushabiki mkubwa wanasema kuachana kwa nyota hao wawili imekuwa ghafla kwani majuzi (jumapili) McIlroy alichapisha picha yao wawili wakila chajio katika mkahawa mooja wa kifahari mjini Monte Carlo.
Wawili hao waliopewa jina la utani la pamoja la 'Wozilroy' waliwaduwaza mashabiki wao walipoanza usuhuba mwaka wa 2011 baada ya kukutana katika mechi ya masumbwi.
0 comments:
Post a Comment