Watu 9 wameripotiwa kuuawa katika majengo ya wizara ya elimu
mjini Mogadishu,Somalia.
Wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo
kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami
kwa bunduki za rashasha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa
Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab,
amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa
''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara
ya elimu''
Mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya
majeshi ya serikali na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa
polisi.
Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya
katika siku za hivi punde.
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja
mjini Mogadishu
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja
mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .
Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo
wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya
risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo.
hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al
shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo.
Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa
mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.
0 comments:
Post a Comment