Facebook

Sunday, 26 April 2015

Uchambuzi wa mechi kali za leo Ligi Kuu Uingereza.

Everton vs Man United 14:30
   Tukianzia katika mchezo wa mapema kabisa majira ya sa 14:30 vijana wa Martinez ambao wamekumbuka shuka pamesha kucha watakwaana na Man Utd.
     Licha ya matokeo mazuri ya hivi karibuni bado hali si shwari kwa Everton kwani mpaka sasa wapo nafasi ya 12 kwa pointi(41) kulingana na uwezo mkubwa walio uonesha msimu uliopita wengi tulitaraji kuiona miongoni mwa timu zinazo wania nafasi ya nne, ukiachilia mbali majeraha mengi katika kikosi cha kwanza lakini msimu huu timu imekosa muunganiko mzuri hasa safu ya ulinzi na kiungo kitu kilicho pelekea kuwa hapo walipo.

   Mbele ya Utd ambayo imetoka kupoteza dhidi ya Chelsea kazi ya ziada itahitajika kwa vijana wa Goodison Park ukiachilia mbali takwimu nzuri walizo nazo katika mechi 2 kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Utd ( 1-0 August) 2012  ( 2-0 Aprl 2014) ila bado watahitaji kazi ya ziada kwenye mchezo huu walau wapate pointi kwani pindi wanashinda michezo hiyo walikuwa vyema zaidi ya msimu huu.

    Wamecheza mechi 33 W-10,D-11,L-12, huku waki funga magoli 41 na kuruhusu 43 wana asilimia 27% za kutoruhusu wavu wao kuguswa kwa hizo takwimu inaonesha ni jinsi gani ushindi ni hafifu.
     UTD waliocheza michezo 33, W-19,D-8,L-6, wakiwa na pointi 65 mpaka sasa upande wao wamefunga magoli 59, huku wakiruhusu magoli 31 na wana asilimia 30% za kutokuruhusu nyavu zao kuguswa kikubwa upande wao ni nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulays msimu ujao licha ya kufungwa na Chelsea baada ya mwendelezo mzuri wa matokeo bado wamekuwa na mchezo mzuri.
   Licha ya majeraha wengi waliokuwa nao katika kikosi cha kwanza bado walionesha uwezo mbele ya Chelsea kitu kinacho pelekea kuwa na nafasi mbele ya Everton, watahitaji kuzuia kutokujirudia kwa ile historia ya 1987 ya kufungwa mfululizo na Everton ktk dimba la Goodison Park.
     Uwepo wa Evans anaerejea baada ya kifungo kutokana na sakata lake na Cissé kutakuwa nguvu kwenye safu ya ulinzi ya Van Gaal vilevile kwa RVP.
     Mchezo uliofanyika Old Trafford Everton alifungwa 2-1 lakini pia endapo watafungwa na United watakuwa wamefikia rekodi ya A.Villa ya kufungwa mara nyingi zaidi (32) dhidi ya Manchester.
     Katika michezo ya ugenini Utd si wazuri sana kwani kwenye mechi 9 wameshinda 3 sare 4 na kupoteza mara 2 na ukija pale katka dimba la Goodison Park ukiachilia mbali kupoteza mechi mbili za hivi karibuni bado Manchester wana ubavu kwani kwenye michezo 22 ya Ligi hivi karibuni Utd W-14,D-3,L-5 wakifunga magoli 39, wakiruhusu 23 na mara 8 hawaja ruhusu goli.
     Wenyeji wao Everton mambo yapo hivi wakiwa dimba lao dhidi ya Utd W-5,D-3,L-14 wakifungwa goli 39 huku wakifunga goli 23 hawakuruhusu goli mara 4.
    Ngoja tusubiri kama ni Lukaku ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanne walio ifunga Utd hat-trick wakiwemo kina Kuyt,Bentley na Etoo ama ni kina Mata na Rooney kwenye mchezo wa 170 kati ya timu hizi huku katika michezo 169 kwa ujumla Utd akishinda 76 dhidi ya 53 za Everton.

-----------

    Tukihamia katika Jiji la London miongoni mwa majiji yenye mvuto wa aina yake huku likiwa lina timu nyingi ktk ligi (6)  kutakuwa na bonge la mechi ambalo ni zaidi ya kutafuta pointi ni kati ya

      ARSENAL 18:00 CHELSEA

   Kama mchezo wa awamu ya kwanza ambapo tulishuhudia makocha wa timu hizi wakitaka kunjana sijui nini kitatokea kwenye mchezo ambao Mourinho atahitaji kumfanya Mzee Wenger kama moja ya kipachi cha ngazi kuelekea ktk jukwaa la kuchukua ubingwa wa Epl.
    Ni siku nyingi wana Arsenal hawaja kenua mbele ya Chelsea kwani mara ya mwisho ni 2011 walipo livunja Daraja kwa ushindi wa goli 5-3 Van Persie akipiga tatu huku moja ya tukio la kuvutia likiwa kuteleza kwa John Terry.
    Tangu hapo mambo huwa magumu kwa Arsenal ktk kuzipata pointi tatu kwa Chelsea kosa kubwa ambalo limekuwa likiwagharimu ni kutokuwa makini kwenye safu ya ulinzi.
   Mchezo uliopita Arsenal dhidi ya Chelsea walirudia historia ya mwaka 2003 dhidi ya Utd pale OT ya kutokupiga shuti lililo lenga goli kitu ambacho kilionesha ni jinsi gani safu ya ushambuliaji ilikuwa na kutu.
    Ukiachilia mbali majeruhi kwa pande zote huku hali ya Mertesacker ikiwa haijulikani na upande mwingine wa shilingi kumkosa Costa labda achezeshwe kiulazima bado si sababu ya timu zote kutokupata matokeo.
   Hivi sasa kila upande umekuwa na matokeo mazuri sana Arsenal pointi 66 Chelsea vinara pointi 76 kinacho onekana kuwabeba Arsenal mbele ya Chelsea hivi sasa ni uchezaji mzuri ndani ya uwanja ingawa upande wa Chelsea hawa angalii kucheza vyema zaidi ya kulenga shabaha ya pointi tatu muhimu.
    Hii ni vita kubwa ki mpira ktk mchezo huu wote wakitumia 4-2-3-1 na kwa namna ya uhalisia mbinu za ziada kutoka kwa wachezaji au makocha ndo zitaamua nani mbabe.
     Mourinho anahitaji pointi kuelekea kuchukua ubingwa pia kingine atahitaji kuendeleza ubabe wake kwa mzee Wenger kwani mara 12 amemfunga mechi 7 na kutoa sare 5 hivyo hivyo kwa upande wa Wenger atahitaji kufuta historia hiyo mbaya pia kurejea nafasi ya pili baada ya City kushinda dhidi ya Aston Villa.
    Kwenye michezo 12 ya hivi karibuni Arsenal kashinda mara 2 ambazo Mourinho alikuwa kasha timka zake Darajani huku wakipoteza mara 8 na sare 2.
    Si vita ya Pointi au ya makocha bali kuna vita nyingine tena mbili ya kwanza ni Fabregas ( Fabrepass) huyu ndiye mchezaji anae ongoza kwa kutoa pasi za mwisho za magoli Epl (16) atakuwa anarejea nyumbani ambapo atahitaji uvumilivu mbele ya zomeazomea ya mashabiki wa Arsenal kutokana na kuikacha Arsenal pindi walipo kuwa wanamtaka na kuelekea Darajani kwa kigezo cha kunyanyua makwapa ( kuchukua vikombe).
   Vita vingine ambavyo vitakuwa kwa wachezaji ambao wanawania tuzo ya mchezajo bora wa msimu pia wamekuwa wakisababisha maneno mengi kwa fans wa Arsenal na Chelsea si wengine bali ni Hazard na Sanchez, hawa wote wamekuwa na umuhimu mkubwa kwenye vikosi vyao.
    Hazard ambae mpaka sasa anamagoli 13 na pasi za magoli 8 amekuwa akizungumzwa kama ni miongoni mwa wachezaji bora wa Dunia wanao staili kuchukua Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ukiwaondoa Messi na Cr7, amekuwa aki ibeba timu mara nyingi na kumzuia kwake inakuwa moja ya njia za kuizuia Chelsea kupata matokeo.
     Sanchez yeye mpaka sasa anagoli 14 huku akitoa pasi za magoli 8 amekuwa ni msaada mkubwa kwa Mzee Wenger msimu huu ni msimu wake wa kwanza Epl na kwa kiwango anacho onesha wana Arsenal wataraji makubwa toka kwake kama atazidisha juhudi.
     Mchezo utakuwa ni undava-undava hasa kwa upande wa Chelsea ambao ukiachilia mchezo mzuri wa kufunguka walio anza nao msimu huu asilimia kubwa tangu mwaka uanze wamekuwa wakicheza kwa kujihami hasa wakitumia viungo wao walio wazuri ktk kukaba.
   Usishangae kumuona Zouma hivyo kina Cazorla na Coquelin watahitaji kazi ya ziada kupenya katika nusu ya Chelsea ambao kwenye michezo 6 dhidi yao hawajafunga goli.
    Arsenal kutokuwepo kwa Costa safu ya ulinzi itaweza pumua ingawa uwepo wa Drogba ambae ktk michezo 14 amefunga mara 13 anaweza kuwa tishio kwa kutaka kuendeleza takwimu nzuri dhidi yao achilia mbali umakini hasa utahitajika kwa Hazard.
    

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment