Facebook

Tuesday, 28 April 2015

HIZI NDIZO FAIDA ZA KUNYWA MAJI MWILINI

1: Kupunguza uzito: Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito,
kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari.

2: Afya ya moyo: Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari
ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa
Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji
zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na
ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2
au chini ya hapo.

3: Nishati ya mwili: Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie
mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye
nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama soda,
juisi au bia.

4:Tiba ya kichwa: Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja
na kuumwa kichwa. Kunywa maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana
na kuumwa kichwa mara kwa mara.

5:Ngozi nyororo: Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza safisha
ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo.

6: Matatizo ya choo: Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo,
kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu
wa choo mara kwa mara.

7: Usafishaji wa mwili: Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa
uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.

8: Saratarani: Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji,
kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo
wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya
kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa
saratani ya kibofu cha mkojo.

9: Mazoezi: Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe
na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida
ya mazoezi ipasavyo.

0 comments:

Post a Comment