Jana baada ya kuona Majina ya wachezaji katika mechi ya Arsenal na Liverpool niliona vitu viwili kwa haraka haraka, kwanza ni makocha kuwapanga watu wawili wenye bahati nzuri na timu zao msimu huu!!,
Kwa Arsenal alikuwepo Ozil na kwa liverpool alikuwepo Lucas Leiva.Ozil tangu arudi kutoka Majeruhi kwenye mechi alizocheza Arsenal wamechukua Alama 27 kati 30 ukijumlisha na Alama za mechi ya Jana kwa Upande wa Lucas , kwenye mechi zote alizoanzishwa za ligi mwaka liverpool haijawahi kupoteza.
kwa kuangalia hivyo utaona ni njinsi gani wachezaji hawa wanabahati ya matokeo mazuri na timu zao!!, nilisubiri kuona nani ana nyota kali!!, kwenye mechi ya kwanza kati liverpool na Arsenal , lucas ni mmoja wa viungo waliocheza vizuri sana siku ile, Dakika 15 za mechi ya jana Lucas alikuwa anapoteza mipira mingi kwenye eneo la timu yake , hii ilisababishwa na vitu viwili vikubwa , cha kwanza Viungo wa Arsenal katika dakika 15 za mwanzo walikuwa kwenye kiwango cha juu na hii ilitokana na lengo lao la kupata goli la mapema na hii ilitia hofu kwa viungo wa liverpool hasa hasa Lucas aliyepoteza mipira mitatu ya wazi kwenye robo yake.
kitu kingine kilichosababisha Lucas asiwepo kwenye kiwango chake kulinganisha na mechi ya Liverpool na Arsenal pale Anfield ni kuwepo nje ya uwanja kwa muda mrefu , ilikuwa karata iliyoshabihiana na karata aliyocheza Big Sam kwa Wiston Reid aliyekuwa nje kwa majeraha na mwisho wa siku karata yake kutofanikiwa na Reid kupata kadi ya njano.
Kitu kingine nilichokiona baada ya kuona orodha ya wachezaji ni baada ya kumuona Toure. Nilisubiri kuona kama Toure ataweza kupangua maneno yangu niliyosema siku baada ya Martin kupewa adhabu na FA ya Uingereza kuwa kuna madhara makubwa kama Toure Akipangwa kama beki wa kati kama mtu wa kuziba pengo la Martin, nilisema kwa kuziba hili pengo lazima liverpool wangebadili mfumo kutoka ule wa kuchezesha mabeki watatu mpaka mabeki wanne, Martin ndo mhimili wa mfumo wa mabeki wa tatu pale Liverpool, kweli nilichotegemea ndo kilichotokea, Toure hakuwa kiongozi kwa Can na Sakho hasa hasa kipindi cha kwanza, pia hakuendana na kasi ya mchezo , angalia goli la Sanchez , Giroud kitu utakachogundua Toure hakuwa mtu sahihi kuziba pengo la Martin, kipindi cha pili Brendan Rodgers aliamua kuchezesha mabeki wanne , Sakho akawa na Toure hii ilisaidia kiasi fulani kupunguza makosa binafsi ya Toure , ila kama Toure angeendelea kucheza kama beki pekee wa kati basi Arsenal walikuwa na uwezo wa kuzirudisha goli 8 walizowahi kupingwa na Manchester united.
Tukiizungumzia Manchester United, Kwa mtazamo wangu unaweza ukaifananisha na duka linaloshindana na maduka mengine.
Carrick ndo Afisa mipango wa hilo duka yeye ndo anakuja na mipango jinsi gani duka liendeshwe , Herrera yeye ni wale kwenye Filamu tunawaita " STORY DEVELOPER "
Baada ya kupokea mipango ya bwana Carrick yeye ndiyo anaiendeleza na kuikuza ile mipango yeye ndiyo anayeamua Bidhaa yani "Mipira" iende wapi kwa Mata,Young na Rooney.
Fellaini ni jambazi mvuruga mipango,lililoajiriwa kwenye duka la bwana Van Gaal, Jambazi hili hufanya kazi moja, ya kwenda kwenye maduka jirani ambayo ni washindani wake na kuwabadilishia bidhaa zilizo na soko kwa bidhaa zisizo na soko kwa mfano, Kuchukuwa Whitedent na kuwawekea AHA.
Ukiangalia upande wa kushoto kwa Manchester United, utamuona Evra mweupe, Ila wanatofauti ndogo sana na Evra mweusi huyu mweupe anakaba vizuri kwa akili afu anashambulia kwa tahadhari na kwa akili nyingi, Evra mweusi alikuwa anakaba na kushambulia kwa kasi kubwa kuzidi huyu Evra mweupe ambaye ameleta uhai eneo la kushoto la Manchester united kwa siku za hivi karibuni.
Tofauti na Chenga zake, Kuminya mabeki lakini Young hana madhara makubwa ukilinganisha na Di Maria, Kuna kipindi Di maria akiwa uwanjani unaiona Manchester united hatari, Young krosi zake nyingi hazimfikii mshambuliaji,
Di Maria krosi zake nyingi zinazmfikia mshambuliaji.
Kuna Faida kubwa kuwaanzisha wote Mata na Di Maria kuliko kuwaanzisha Mata na Young.
Chelsea wamekuwa watumwa wa ligi huwezi kuwatofautisha na QPR, BURNELY, LEICESTER CITY, wamekuwa wakitumia nguvu nyingi ili kupata matokeo, nguvu walizotumia kwenye nusu ya msimu huu zimeongezeka sana na huku wachezaji wao wengi waliotumika sana msimu huu kuonekana kuchoka, kama ulibahatika kuangalia mechi dhidi ya Burnely waliyotoka sare, mechi dhidi ya Hull City waliyoshinda 3-2 na hii ya Jana dhidi ya Stoke wamekuwa wakitumia nguvu nyingi sana hasa hasa wakitizama nyuma moto wa Manchester city na United, na Arsenal.
Kuna kitu kimoja unatakiwa ukifahamu , mambo anayoyafanya Hazard yameshafanywa kipindi cha nyuma na J.COLE kipindi cha Claudio Ranieri wanachotofautiana ni kitu kidogo , wimbo wa Hazard unaimbwa sana midomoni mwa watu!!, ilihali wimbo wa J.Cole haikuimbwa sana midomoni mwa watu.
Kati ya mtu ambaye atakula pasaka na tumaini jipya la kutokushuka daraja wa kwanza kabisaa ni kocha wa Leicester city Nigel Pearson wa pili basi ni yule wa QPR.
Pasaka njema wapendwa ngoja mimi nibaki naburudika kuangalia marudio ya magoli ya Giroud, Sanchez, Ozil, Adam , Esteban Cambiasso, Zamora , Gomis , Rooney,Herrera,Vargas.Ndo magoli bora kwangu yaliyofungwa jana,nkimaliza magoli nitamalizia na saves za Tim Howard
Ahsanteni Mungu Awabariki.
#Martin kiyumbi.
0657771077
0 comments:
Post a Comment