Saturday, 11 April 2015
"NATAMANI TERENCE TAO ANGEKUWA MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA."
Nini unakumbuka Unaposikia mtu akimtaja Hector Cuper? Hapana shaka Kumbukumbu zako zitarudi mpaka miaka ya nyuma kidogo kuanzia 1997 -2002.
Hapo ndipo Utaiona Mallorca na Valencia kwenye kichwa chako.Ubongo wako utafanya kazi kubwa sana ya kukuletea Mallorca bora iliyopoteza kwenye Fainali ya kombe la Washindi ulaya ( UEFA CUP WINNERS ) , Ubongo wako hautoishia hapo tu kwani utakukumbusha Mallorca bora ikipoteza kwenye fainali ya Copa Del Rey dhidi ya Barcelona 1997. Ukiuruhusu zaidi ubongo wako utakukumbusha Valencia iliyofika mara mbili fainali ya UEFA CUP na mara zote ilipoteza !!, Mara ya kwanza dhidi ya Real Madrid 2000 na Mara ya pili zidi ya Bayern Munich 2001 kwa mikwaju ya penalti!!, Chini ya kocha mwenye bahati mbaya na michezo ya fainali Hector Cuper naamini baada ya kulikumbuka hili jina ubongo wako utatembea mbele kwa kasi mpaka mwaka 2015 na hapo utamalizia kwa kushusha pumzi baada ya kugundua Hector Cuper ndio Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Misri. Timu ambayo tupo Kundi moja kwenye mashindano ya kufuzu AFCON 2017 Yatakayofanyika GABON.
Kwa haraka ukiliangalia kundi letu lazima kiubaridi cha uoga kipite kwenye ngozi yako.
Ni kundi ambalo timu zote yani Chad , Tanzania, Misri na Nigeria hazikuwepo kwenye michuano iliyopita iliyofanyika Equatorial Guinea.
Chad ambao ndo wanaonekana kama watakuwa vibonde wetu na tumesahau kwamba walikuja kwetu 2014 na wakatufunga 1-0 pia Chad hawa hawa ndo mabingwa wa CEMAC Michuano inayoshirikisha wachezaji wa ndani kutoka Equatorial Guinea , Chad , Cameroon ,Jamhuri ya Congo,Gabon na Afrika ya kati, hii inaonesha Chad hawatakuwa wateja kwetu kama tunavyofikiria.
Kwenye akili ya wachezaji wetu naamini watakuwa wanazihofia Nigeria na Misri.
Hofu hii ndiyo imenifanya nimkumbuke mwana HISABATI mkubwa duniani , mwanadamu anayesadikika kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria kuliko wanadamu wote duniani TERENCE TAO.
Naamini kama leo hii TERENCE TAO angezaliwa Tanzania kwenye kizazi cha leo cha Timu ya Taifa na kama angebahatika kuwa mchezaji wa timu ya Taifa naamini asingekuwa na hofu ya aina yoyote juu ya kundi tulilopangwa.
Pamoja na kwamba Timu yetu hii imeandaliwa kwa mawazo duni ya Jana tukitegemea kuona bora yetu ya kesho, naamini hili lisingemtatiza hata kidogo, kitu ambacho angekifanya ni kimoja tu.Angetumia uwezo wake mkubwa wa kufikiria na uwezo wake mkubwa wa kufanya hesabu ili aitengeneze kesho yake nzuri. Naamini asingekubali kujiona akiendelea kuonekana kwenye kioo cha AZAM TV , akili yake ingehitaji kuona haja kubwa sura yake na miguu yake ikionekana kwenye Vituo vikubwa vya TV duniani huku akiteleza kwenye nyasi bora baada ya kufunga goli.
Kuwepo kwenye kundi hili TERENCE TAO , Kundi ambalo vigogo wa AFRIKA wapo kungemfanya akumbuke kuwepo kwa mawakala mbalimbali wa soka barani ulaya watakaokuja kuangalia vipaji vya NIGERIA na MISRI na hapo hapo angefanya mahesabu makubwa ya kugeuza akili za mawakala, Badala ya kuwaona wachezaji kutoka MISRI na NIGERIA naamini kupitia mahesabu yake angeonewa yeye.
Vyombo vingi vya habari vitaweka camera zao uwanjani kwa sababu ya NIGERIA na MISRI , kwa hesabu za TERENCE TAO zingemnufaisha kwa kupata mikataba mingi ya Matangazo.
TERENCE TAO angeona huu ndo wakati wa kuchukia kucheza kwenye viwanja vibovu, angeona ndo muda wa kuchukia kucheza kwenye timu zetu chini ya mishahara midogo, ndiyo muda wa kuchukia kupigwa picha kwa camera za Canon na waandishi wa habari waliorundikana nyuma ya goli.
Angeona ndo wakati wa yeye kupata mashabiki kutoka Chad, Misri na Nigeria kwa jitihada zake nzuri ili atengeneze ukubwa wa mashabiki kwa faida ya biashara atakazozipata baada ya makampuni mbali mbali kumuona mjini Cairo au Alexandria au mjini Lagos au Abuja , au mjini N'Djamena .
Na mwisho wa siku uwezo wake wa Hesabu ungeifanya timu yake ya Taifa iende nchini GABON 2017.
Imeandaliwa na ........
Martin Kiyumbi.
0657771077
0 comments:
Post a Comment