Ifike mahali siasa zipigwe marufuku vyuoni.Migomo ni miuri kama itafuata taratibu kuhalalisha migomo hiyo na sio kutumiwa kwa ajili ya kunufaisha watu au kikundi fulani.Kuna siku uongozi
wa kwenye taasisi za elimu na elimu ya juu ziwe ni kazi (ajira) maalumu.Haya
mambo ya maandamano pamoja ni haki za wanafunzi yanapoteza malengo na kuwatia
hasara wengine za maisha.Inauma sana siku kadhaa zimepita kuna wanafunzi kadhaa
wamepoteza miasha na wengine wamejeruhiwa.Sasa hivi wazazi wa hawa vijana watafaidika
vipi na matunda ya vijana wao waliowasomesha kuanzia walipokuwa wadogo hadi
kufikia ngazi ya chuo,taifa linapoteza nguvu kazi, Inauma sana.
Taifa linapoteza vijana kwa mambo ambayo yangeweza kufanywa
kwenye harakati za siasa za mtaani. Jamani kuna muda wa kufanya na kuna muda wa
kujiandaa kufanya. Tukiwa vyuoni huko tuwe tupo kwenye kujiandaa kufanya, na
shule ikiisha ni muda wa kufanya.Najua kuna wengine wameathrika zaidi ya hivi
hata kama mwili hawakuumia.Huku Taarifa zilizopo kuna wanafunzi amefariki chuo
Kikuu cha Dodoma,matatizo ya pale yanayatatulia kinyume na taratibu,wanaoharibu
taratibu hizi ni viongozi wanaosimama kama wawakilishi wa wanafunzi tatizo ni siasa
tu,vyama vya siasa vinaharibu utaratibu chuo vyuo hususan Chuo Kikuu cha Dodoma,ambapo
umetokea mgomo kwa wanafunzi wanaochukua stashahada katika chuo hiko.
Siungi mkono jeshi la Polisi kuhusika na mauaji ya aina
yoyote ile.Ila nawaomba vijana wenzangu mliopo katika vyama vya siasa muyapime
maneno na maagizo ya viongozi wenu kwa faida ya taifa hili.Kunu huyu ambaye ni
kiongozi pale Chuo Kikuu cha Dodoma anaitwa Mwakibinga.Huyu Mwakibinga zaidi ya miaka 4 aliyokaa nje ya chuo Kikuu
cha Dodoma.Hakika palitulia siku za hivi karibuni amerudishwa Chuoni ameanza
tena na kuwa sehemu ya kusababisha mauaji ya mwanafunzi wenzake.
Aliyekuwa Waziri Mkuu Philipo Mwakibinga
"Academic
institution is a place to learn not to practice politics although politics is
tought” .Ni maneno ya mwalimu wangu
aliyokuwa ananiambia mara kwa mara nilipokuwa nachukua masomo yangu ya
sekondari katita shule ya sekondari ya St.Matthew’s
Waziri mkuu wa chuo Kikuu cha Dodoma Philipo Mwakibinga huyuhuyu,anatumia
chuo kama sehemu ya kujijenga kisiasa, ni mtu ambae hana malengo na taaluma
yake,hana nia wala malengo na anaowaongoza bali ni mtu mwenye maslahi binafsi,mgomo
uliotokea Chuo kikuu cha Dodoma yeye ndie aliyeupika kwa siku sita na usiku wa
saa sita kabla ya mgomo huo kutokea ndipo alipofanya kikao cha mwisho cha
maandilizi ya mgomo na madhara yake ndiyo haya,wanafunzi wenzake wamepoteza
maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa.
Na alifanikiwa kuwalaghai wanafunzi wa stashahada na kuleta
haya yaliyotokea,ni maagizo moja kwa moja kutoka kwa wale anaofanyanao kazi kwa karibu,na
mgomo huu ilikuwa ajenda ya kikao chao cha tawi walichokifanya kijijini
Ng'ong'ona Jumapili ya tarehe 4.
Siasa kwenye vyuo inapoteza malengo ya vijana wengi sana.
TusemenI kweli na tuache mahaba ya vyama vyetu. Sikatai wanafunzi kugoma, wote
tumekuwa wanafunzi, ila ifike mahali tutazame njia za kutafuta ufumbuzi wa haya
yanayotupelekea kugoma. Sasa hapa kwenye huu mgomo ukifanya upembuzi yakinifu
kati ya faida na hasara utagundua hasara ni kubwa kuliko faida.
Miongoni mwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma aliyeumizwa vibaya na Polisi
Polisi wanaweza kuwa walitumia nguvu zaidi kitu ambacho
sidhani kama ni jamnbo zuri katika kutawanya na kutatua matatizo.Ila kwa nini
wanafunzi wahamasishwe kufika huko? Africans are incapable of sustaining their
protests in two days" Prof. Patrick Lumumba
Lakini kwa upande wa pili,serikali hii iliingia dosari tangu
katika uchaguzi wao,waliweka siasa na itikadi zao mbele kuliko lengo kuu la wao
kuwafanya kuwa pale,mzizi ni mmoja tu,kuondoa ushabiki na kufuta kabisa uwepo
wa maswala ya vyama vyuoni.
Kila mtu anajua maafa na hasara ya maandamano lakini tukubaliane kwamba mifumo yetu pia inachangia sana kuwalazmisha vijana kufanya hivyo.Ufaranza juzi walikuwa na maandamano makubwa, Ukraine mwaka jana wamekuwa na maandamano takriban miezi miwili. Tumeshuhudia migomo na maandamano ya kuondoa tawala mbovu kwenye nchi za kiarabu, Brazil na USA migomo ipo.Lakini nchi ndogo kama Tanzania ambavyo hazitambui maana halisi ya migomi katika mfumo utawala wa kidemokrasia matatizo kama haya yanatokea.
Kila mtu anajua maafa na hasara ya maandamano lakini tukubaliane kwamba mifumo yetu pia inachangia sana kuwalazmisha vijana kufanya hivyo.Ufaranza juzi walikuwa na maandamano makubwa, Ukraine mwaka jana wamekuwa na maandamano takriban miezi miwili. Tumeshuhudia migomo na maandamano ya kuondoa tawala mbovu kwenye nchi za kiarabu, Brazil na USA migomo ipo.Lakini nchi ndogo kama Tanzania ambavyo hazitambui maana halisi ya migomi katika mfumo utawala wa kidemokrasia matatizo kama haya yanatokea.
Sidhani kama sakata kama la ESCROW lingetokea kwenye nchi
inayojielewa watu wangefyata mikia. Sidhani Kama kweli tunachukia maandamano na
migomo tuanze kwanza kukemea na kulaani vyanzo vyake.
Nafikiria kuwa hivi vyeo vya kiserikali vifutwe. Tuwe na mwenyekiti
na mlolongo wa viongozi wengine ukifuata ili kuondoa kiburi. Lakini pia
wanafunzi wanapaswa kujua wametumwa na jamii vyuoni kuhenyea chakula cha kijiji
si chao binafsi na wazazi wao. Vyuoni kuna somo liitwalo ‘Political science’ tunaweza
kusoma na kisha kuja kufanyia mafunzo ya vitendo uraiani baada ya masomo ili
vyuo viwe mahala patulivu.
Maandamano ni kweli njia ya kupaza sauti ya pamoja lakini
hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kuwa maandamano yameleta tija.Nimetolea
mfano mapinduzi ya Waarabu kupitia maandamano na kasha kufanya maoinduzi ‘Arab
Spring’ mfano Libya,Tunisa,Misri n.k .Hivi leo hii ni kweli Waarabu wanafurahia
maamuzi yao? Libya hivi sasa wako katika kipindindi kigumu zaidi katika
historia yao, nchi haina amani ya kweli tangia alipoong’olewa Gadaffi
madarakani.
Libya,Brazil,Ufaransa binafsi naamini katika majadiliano
zaidi ambayo najua ni suluhu isiyoshindikana wakati Mugabe anatoka porini
kusaka Uhuru alikuja kwa Mwl Nyerere kuomba ushauri.
Yeye alitaka kurudi
msituni.Mwl Julius Kambarage Nyerere akamwambia
"kaa na wazungu mzungumze, ukirudi porini nawaambia nchi za frontliners
wakutose" Mugabe akamuelewa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nguvu ya
mazungumzo ya hoja. Wazungu wakataka kumuweka kama Rais huku akiwa na waziri
mkuu ambaye ni mzungu hilo nalo akakataa.Akataka Urais wenye mamlaka
kamili.Kupitia hili nadtumai unaweza kujifunza ulevi wa madaraka unapoitwa Rais.
Uenyekiti kidogo hupunguza hisia za kifalme. Ndicho kinachotokea katika klabu
kubwa mbili nchini Simba,Yanga pamoja na shirikisho linalosimamia mpira wa
miguu nchini TFF. Umungu mtu.
Lakini tusistajaabu sana hiyo ni hulka ya mwanadamu,wapo
ambao hawawezi kujifanya miungu watu! Che guevara baada ya kuleta ukombozi nchini
Cuba na kuwa waziri baadae aliachia ngazi na kujivua vyeo vyote alivyonavyo ili
akalete ukombozi wa dunia.Hoja yangu kubwa ni kuwa wapo viongozi ambao wataweza
kuishi na kutenda kutokana na taratibu za vyuo husika na tunayo mifano ya
kutosha.Napenda sana kuwa kama sheria inavyotajwa na wahenga kama msumeno ambao
unakata huku na huku.
Katika kulitatua tatizo hili ninatoa mapendezo mbalimbali na
miongozo mbalimbali ambayo ikitekelezwa baadhi inaweza kutuletea ufumbuzi
sahihi.Migomo hata kama kukiwa na wenyeviti kama hatutafuti ufumbuvi wa
matatizo ya wanafunzi ni ngumu sana kuisha.Rais wa Chuo Kikuu cha Dodoma anatoa
tamko dhidi ya serikali anapata wapi hii nguvu kuna baaadhi ya mambo nampongeza
sana Rais Jakaya Kikwete nadhani yeye ni miongoni mwa viongozi pekee Afrika
Mashariki aliyeachia uhuru wa kijieleza popote pale sasa hivi hata madaladala
nayo yanagoma,ni juzi tu hapa kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimoja
kikubwa nchini Nchi aliadhibiwa kifungo baada ya kuyachambua madhaifu ya Rais wa
nchi hiyo Uhuru Kenyatta na kasha kuyaweka hadharani,nadhani huu uhuru
unatumiwa vibaya sana na vyama au watu.Hao wa Chuo Kikuu cha Dodoma ukichunguza
kiundani ni siasa tu ndani yake tatizo
ni dogo hao watu waliopewa dhamana ya kushughulikia matatizo ya wanafunzi
nadhani hawakufanya kazi yao ipasavyo.
Tuseme ukweli kati ya wanavyuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma na
serikali ni nani ameadhirrika zaidi? Ifike mahali tupime maamuzi yetu kama yana
afya au la! Hivi kweli wewe mwanafunzi umetoka kijijini huko ambako hata barabara
haifiki kuipata barabara kuu ni mtihani!! Familia uliyotoka unaijua vyema
maisha yalivyo, leo umebahatika nafasi ya kusoma marejesho yake ni migomo hivi
hapa unamkomoa nani? Haya leo hii umepata kilema cha kudumu mzazi wako anao
uwezo wa kukutibia ? Haya umefukuzwa unaye wa kututetea? Tuachane na wanasiasa
someni mmalize kisha nendeni kwenye ulingo wa siasa kama mnaitaka kweli!
Hao
wanasisa walitulia, wakasoma na si kwamba kulikuwa hakuna matatizo la hasha lakini
unaangalia kipaumbele chako !
Wanavyuo wa siku hizi hawashikiki wao kila jambo wanajua
nadhani lingekuwepo somo la kujua askari akisema tawanyikeni ukikaidi ujue nini
kinafuata zaidi ya virungu na mabomu ya machozi ni mawazo yangu tu. Inauma sana
mtoto umemsomesha kwa taabu kubwa mno halafu anakwenda kujiingiza kwenye vitu
vya hovyo visivyomjenga! Taarifa rasmi zinasema uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma
(UDOM) umeazimia kumfukuza chuo moja kwa moja waziri mkuu wa serikali ya
Waziri Mkuu Bwana Mwakibinga mwanafunzi wa “College of
humanities and social sciences” ambaye aliwahi
kusimamishwa chuo kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuruhusiwa kurudi
chuoni na kuendelea na masomo. Mwaka jana baada ya miaka kama 3 alirudishwa
chuoni na baadae kuingia tena katika siasa ambapo aliteuliwa kuwa Waziri mkuu
wa kitivo hicho. Juzi umeibuka tena na mgomo.
Akiwa raisi aliruhusu mgomo wa college yake baada ya wizara
ya elimu kutoa maelekezo ya namna watavyoshughulikia suala la field utaratibu
ambao yy na serikali yake hawakukubali. Nakumbuka makamu mkuu wa chuo alikuja
saa sita usiku kuwasihi wanafunz waendelee na masomo na walifanya mazungumzo na
uongozi wa chuo lakini serikali ya wanafunzi hawakusitisha mgomo.
Siasa inavuruga sana vyuo nchini.Lakini serikali nayo
inatengeneza bomu linalowalipukia wao wenyewe.Hawa wanafunzi walioko vyuoni
wengi wao hawana mikopo mwisho wa siku inapelekea wanafunzi waishi maisha
magumu sana huku wengine hususani wabinti inafikia hatua wanajiuza miili you waweze
kupata pesa ambayo itawasaidia wajikimu na kuendelea na masomo.
Binafsi naamini
njia pekee au ‘muarobaini’ wa matatizo makubwa katika vyuo vyetu ni kuhakikisha
serikali inawapa mikopo wanafunzi mbalimbali.Serikali inaweza ikadhibiti mianya
iliyopo inayosababisha ubadhilifu mkubwa wa fedha na kusimamia vilivyo sekta
mbalimbali zinazoliingizia taifa kipato hususani kodi na vyanzo vingine
mbalimbali ili ipate uwezo wa kuwahudumia wanafunzi wote waliopo vyuoni na
kuacha kutengeneza matabaka kwa kuwapa baadhi mikopo na kuwanyima wengine ili
hali hawana uwezo wa kuendesha maisha yao ya vyuo nchini.
Nawasilisha hoja……………………………………………………………………
Imeandaliwa na...............
Katemi Methsela
0 comments:
Post a Comment