Saturday, 17 January 2015
TANZANIA NA UKOSEFU WA AKILI
! Nilikuwa najisumbua kufikri kwanini nchi nyingi za kiafrika ni maskini nikajikuta napata jibu moja kwamba tawala nyingi za kiafirika hazina Akili.
Hazina akili ya kutambua umuhimu wa nidhamu katika kuendelea. Akili ya kupambana na maadui wa maendeleo na akili ya kupanga mikakati safi ya maendeleo.
Nidhamu ni muhimu sana katika maendeleo hata ya mtu mmoja mmoja.
Nchi nyingi zilizochelewa kupata uhuru kama Afrika kusini zinaonekana kuwa na hali nzuri kiuchumi ukilinganisha za zile zilizowahi kupata Uhuru kama Tanzania. Kwanini?
Kama mkoloni lengo lake kuu ni unyonyaji(exploitation) na mnyonywaji anaendelea pale anaponyonywa na maendeleo yake huwa hafifu baada ya mnyonyaji kumpa kisogo, Kwanini Tusiamini kwamba Afrika tunakosa akili? Akili ya kuendeleza, Kusimamia na kulinda rasilimali zetu?
Hivi ingelikuwa Tanzania hatuna rasilimali tulizo nazo leo tungekuwa wapi? Tusingekuwa na madini(aina 18), wanyama wa kila aina, vivutio vya kitalii kama mlima kilimanyaro na bonde la ngorongoro, maziwa mito na bahari, kiswahili(lugha yetu) n.k HIVI TUNGEKUWA WAPI KIMAENDELEO??
Hatuna akili na ndiyo maana tumeruhusu mfumo wa kibaguzi ambao hautoi muanya wa maeneo ya nchi kuendelea kwa ushindani na usawa. Kwa Tanzania ni sawasawa kwa rasilimali za sehemu flani kuendeleza sehemu flani hata kama hakuna uhitaji sana. Unakuta sehemu ambako rasilimali inatoka hakuna hata molamu kwenye barabara zake lakini kilichopatikana kinapelekwa sehemu nyingine kwa ukarabati wa rami sehemu nyingine. Ni lazime ifike pahala kama inchi turuhusu maendeleo katika maeneo mengine ya nchi ambayo kwa muda mrefu hayaendelei na kwakufanya hivyo tutapunguza misongamano ya watu kwenye maeneo ya nchi yaliyoendelea.
Wataalamu na wasomi tulionao wanalalamika tafiti wanazofanya kuhusu nchi yetu hazifanyiwi kazi, zipo makabatini. Tumekuwa wavivu hata kusoma mambo ya msingi.
Mataifa mengine yanatamani kuwa na rasilimali kama tulizo nazo na ndiyo maana unaona watu wanatoka Kuwait kuja kuiba kenge ambao tukikutana nao mtaani tunawashambulia kwa mawe. Kama sio ukosefu wa akili ni nini? Tunayo wizara ya rasilimali kwanini wasianze uzalishaji wa wanyama hawa kwa wingi ili ziada iuzwe kwajili ya kuendeleza nchi.
Hivi nchi inayohitaji kuendelea inaweza kuvumilia ujinga wa wachache wasiokuwa waadilifu kumega keki ya Taifa kwa anasa zao. Hii nchi imetekwa na wezi. Iko mifukoni mwa mashetani.
Nikipata sababu nyingine ya umaskini wetu nitakuja tena.
Katika nchi zilizotekwa na tawala zisizokuwa na AKILI, siraha ya myonge ni KURA yake.
MUNGU TUONESHE NJIA SAHIHI TUNAPOENDA KUAMUA MSTAKABALI WA TAIFA LETU MWAKA HUU!
Imeandaliwa na....................
Bob Chacha Wangwe
0 comments:
Post a Comment