Duniani kuna viumbe vya aina mbalimbali ambavyo wengi wetu
tunaamini Mwenyezi Mungu aliviumba kwa ustadi wa hali ya juu sana lakini wapo
wale wanaoamini viumbe hivi vilitokea tu kwa nguvu isiyojulikana lakini mwisho
wa siku tunarudi pale pale kwamba Kuna nguvu ya ziada ambayo wengi tunaamini
Mwenyezi Mungu aliviumba.Kuna viumbe vya ajabu sana vilivyoko baharini na nchi
kavu ama hakika ukistajaabu ya Musa utayaona ya firauni.Mabaharia na wavuvi
wamepata wasaa wa kushuhudia vitu vya ajabu sana ambavyo kwa hali ya kawaida
huwezi kuamini.Vivyo hivyo hata nchi kavu kuna baadhi ya sehemu duniani kuna
viumbe vya ajabu na vya kustaajabisha.
Mfano mzuri ni Misitu ya Amazon iliyoko bara la Amerika ya
Kusini hususan nchi ya Brazil kuna nyoka wakubwa na wanene kuliko wote duniani
wanaojulikana kama Anaconda, ukirudi Tanzania sehemu moja inaitwa Kihansi
mkoani Morogoro kuna Vyura wa ajabu ambao wao huzaa kama binadamu tofauti na
vyura wengine duniani.
Sokwe mtu wanaopatikana hifadhi ya Gombe-Kigoma pekee
dunia nzima.Mnyama mkubwa duniani ambaye anaweza kutengeneza kisiwa cha muda
mfupi ndani ya maji anaitwa nyangumi, ama hakika shughuli ya uumbaji ilikuwa ya
kipekee sana.
Katika uumbaji mwenyezi Mungu aliumba viumbe mbalimbali
kisha akavipa uhai na kila kiumbe kina umuhimu wake hapa duniani.Lakini katika
uumbaji huo Mwenyezi Mungu alitumia maarifa zaidi katika kumuumba mwanadamu
kwani alimpa utashi na kasha akampa mamlaka ya kuvitawala vitu na viumbe vyote
vilivyoko duniani.
Ama hakika binadamu ni kiumbe cha kipekee sana.Lakini
miongoni mwa wanadamu kuna mfanano na utofauti katika baadhi ya mambo moja wapo
ni vipawa, Mwenyezi Mungu amemjaalia kila mwanadamu kipawa chake.Tumezoea kuona
binadamu anayeweza kutumia mkono mmoja wapo kati ya mkono wa kulia au wa kushoto
kwa ufsaha zaidi vivyo hvyo hata katika miguu.
Leo ningependa nikuongezee
maarifa na uweze kuwatambua baadhi ya binadamu wenye uwezo wa kutumia miguu au
mikono yote kwa pamoja,yaani mkono wa upande wa kushoto na mkono wa upande wa
kulia au mguu wa upande wa kulia na wa kushoto kwa ufasaha zaidi. Ama hakika
Mungu ni wa ajabu sana.Kwa lugha ya kigeni na kitaalamu zaidi wanajulikana
kama “Ambidexterity”
Binadamu waliozaliwa na uwezo huo wa kutumia viungo hivyo
kwa ufasaha zaidi ni wachache sana, kwa dunia ya leo takwimu zinaonyesha kati
ya watu 1000 unaweza kumkuta binadamu aliyezaliwa na uwezo huo mmoja.
Kwa
ulimwengu sasa “Ambidexterity” wengi ni wale walizaliwa na uwezo wa kutumia
mkono au mguu wa kushoto kisha wakajifunza kutumia viungo vya upande wa kulia,
kisha wanamudu kutumia viungo hivyo kwa ufasaha zaidi.Mara nyingi inawezekana
binadamu huyo akaanza kujifunza kutumia viungo vya upande wa kulia akiwa mdogo,
shule ambapo mkono wa upande wa kulia unapendekezwa zaidi katika matumizi, kwa
mfano mototo anapozaliwa akiwa anatumia mkono wa kushoto katika kula chakula,
moja kwa moja wazazi wa huyo mototo watamlazimisha kutumia mkono wa
kulia.
Vilevile binadamu anayetumia mkono wa kushoto anaweza
kujifunza kutumia mkono wa kulia kutokana matumizi ya vitu mfano mkasi, opena
na vingine vingi ambavyo vinaleta ugumu katika kuvitumia kwa mkono wa kushoto
moja kwa moja inapelekea kujifunza kutumia mkono wa kulia.
Vilevile binadamu wanaotumia mkono wa upande wa kulia
wanaweza kubadilika na kisha kutumia mikono yote au mkono wa kushoto kutokana na
sababu mbalimbali kama vile ajali, aghalabu anaweza kubadilika na kuanza
kutumia mikono yote kutokana na ufanyaji wa shughuli mbalimbali ambazo
zinahitaji ubunifu wa ziada hasa katika shughuli zinazokuwa na uhitaji wa kutumia mikono
yote miwili kwa mfano wale wanaotumia vifaa kama computer katika “TYPING” hali
kadhalika katika kuogelea, upasuaji, kupiga gitaa, upiganaji wa ngumi yaani
‘boxing’ mchezo wa baseball, mpira wa miguu n.k
HAWA NI BAADHI YA NYOTA MBALIMBALI DUNIANI WENYE UWEZO WA
KUTUMIA MIKONO AU MIGUU YOTE KWA UFASAHA.
MCHEZO WA RUGBY
Jonathan Edwards, huyu ni mchezaji wa mchezo wa rugby anasifika
sana kwa kuupiga mpira wa rugby kwa kutumia miguu yote miwili, hakika ni jambo
la kustaajabisha sana.
MCHEZO WA KIKAPU ‘BASKETBALL’
Katika mchezo wa mpira wa kikapu huko marekani uitwao NBA
kuna nyota mbalimbali waliojaaliwa kipawa cha kutumia mikono yote miwili kwa
ufasaha zaidi, anapotumia mkono wa kushoto na kulia huwezi kuona
tofauti.Kawaida ni kwamba wanapotoa pasi fupi fupi wachezaji wa mchezo huo
hupendelea kutumia mkono ambao ni dhaifu yaani ambao hautumii mara kwa mara.
Lakini imekuwa tofauti zaidi kwa baadhi ya wachezaji kama Kobe Bryant, Kyrie
Irving, Carlos Boozer, David Lee, John Wall, Derrick Rose, Andrew Bogut na
Michael Beasley hawa wanavipawa vya ajabu sana, ukipata wasaa wa kuangalia
mchezo huo utastajaabu namna wanavyoweza kutumia mikono yote miwili kwa
ufasaha zaidi.
Lakini cha kustaajibisha zaidi ni mchezaji anayeitwa Bogut yeye
anamudu zaidi kutoa pasi ndefu na kutumbukiza mpira katika kikapu kwa kutumia
mkono ambao ni dhaifu kwake, mkono wa kushoto kuliko mkono wa kulia ambao ndio
anaoutumia mara kwa mara.Kuna ndugu wawili Marc na Pau Gasol wanauwezo wa
kutumia mikono yote kwa ufasaha zaidi.
Bob Cousy,lijendari wa timu ya kikapu Boston Celtics
ililazimika atumie mkono wa kushoto baada ya kuumia mkono wa kulia alipokuwa
shule baadae akawa anatumia mikono yote miwili.Mchezaji wa kati wa LA Clippers,
DeAndre Jordan anatumia mkono wa kushoto katika kushuti lakini anaruka juu na
kurusha mpira kwa kutumia mkono wa kulia.
MCHEZO WA MASUMBWI ‘BOXING’
Katika mchezo wa masumbwi tumeweza kuwashuhudia mabondia
mbalimbali mashuhuri ulimwenguni mfano Jimmy Floyd Myweather Jr na Mike Tyson
ni mashuhuri zaidi katika kurusha ngumi kwa kutumia mikono yote lakini mikono
yao ya upande wa kushoto ndiyo yenye nguvu zaidi na akibahatika kukupiga ngumi
kwa kutumia mkono wa kushoto pambano linaweza kumalizika mapema.
Vivyo hivyo kwa
mabondia wengine kama Mohamed Ali, Evander wanauwezo mkubwa sana wa kutumia
mikono yao kwa ufasaha lakini mkono wa kulia ndiyo wenye nguvu zaidi.Ukiachana
na mabondia hao kuna bondia aitwae Manny Pacquiao huyu ndiye bondia pekee
mwenye uweze wa ajabu na tofauti zaidi na mabondia wengine kutokana na umahiri
mkubwa alionao wa kurusha makombora ya ngumi kwa kutumia mikono yote miwili kwa
ufasaha zaidi.Huwezi kuiona tofauti anapokuwa anarusha ngumi kama mabondia
wengine kitu amabcho kinamsaidia kupata ushindi mapema zaidi katika mapambano
yake mbalimbali.
UCHORAJI
Kuna makala nilishawahi kuandika iliyokuwa inamhusu Leonardo
Da Vinci, huyu ni miongoni mwa wanadamu wachache waliojaaliwa kuwa na akili ya
ajabu na uwezo mkubwa sana.Naweza kujumuisha vitu vyote kwa kumuita ‘Genius’ kwa
lugha ya kimombo.Aliishi katika karne ya 17.Alikuwa ni mchoraji, mbunifu na
mhandisi mkubwa aliywahi kutokea duniani.
Alichora michoro mbalimbali ya majengo
na kupanga miji mbalimbali mikubwa duniani kama vile Madrid, Paris, Venice,
Lambardy-Italia, Fiorentina, Lens, Nice, Istanbul ama hakika hakuna mhandisi wa
majengo yeyote Yule asiyemjua Da Vinci.Leonardo Da Vinci alijaaliwa kipawa cha
kuchora kwa kutumia mikono yote miwili.Falsafa zake zinatumika hadi leo
hii.
Lakini cha kuvutia zaidi ni mchoraji mwingine anayefuata nyayo za Da
Vinci aitwae Gur Keren amabaye anaweza kuchora kwa kutumia mikono yote miwili
hadi miguu kwa ufasaha zaidi.Ukimfuatilia Gur Keren utashangaa namna anavyoweza kutumia miguu yake yote miwili katika uchoraji.
MCHEZO WA SOKA ‘KANDANDA’
Tukiangazia katika mchezo unopendwa zaidi duniani, ukiwa
umejikusanyia mashabiki katika pande mbalimbali za dunia mpira wa miguu huku
wengine wakiuita soka au Kandanda .Tumeweza kushuhudia vipaji mbalimbali,
vizazi mbalimbali vikija na kupotea kisha kuibuka kizazi kingine.Tumeweza kuona
magwiji wa soka Ulimwenguni kama Pele, Garrincha,Maradona,Gaza, Roger Milla,
Platini,George Weah,Zinedine Zidane Zizzou, Buckenber, Ronaldo,Patrick
Kluivet,Ronaldinho,Rooney, Robert Pires, Zola,Silva,Fabregas,Rosicky, Bergkamp,
Di Mateo, Carlos,Deco, Van Persie, Falcao, Hazard, Eto’o,Drogba,YayaToure,Paul
Scholes, Lionel Messi, Mbwana Samata ‘SamaGoal’ ,Iniesta,Arjen Robben,Kevin Strootman, Xavi, Pirlo,Santi
Carzola na wengine wengi wameweza kuuchezea mpira vile wanavyotakana kufanya
chochote kilecwanachopenda uwanjani.
Lakini wachezaji wengi wamekuwa wakitumia zaidi mguu mmoja
wapo kati ya kusho au kulia na wengi wanaweza kutumia mguu mmoja wapo kwa
ufasaha zaidi na mwingine sio kwa ufasaha zaidi.
Lakini kuna baadhi ya wachezaji wamezaliwa wakitumia mguu
mmoja wapo ama wa kushoto au wa kulia na kisha wakajifunza kutumia mguu ambao walikuwa hawautumii kwa ufasaha
zaidi.Wachezaji hawa wanakuwa na uwezo mkubwa uwanjani katika utoaji wa pasina
kufunga magoli na vile vile wanakuwa na uwezo wa kucheza nafasi na pande
mbalimbali uwanjani.
Wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Wesley
Sneijder,Xavi,Iniesta,Fabrigas, David Villa, Hernanes, Zinedine Zidane,Ross
Barkley, Marek Hamšík, Adel Taarabt, Jack Rodwell, Adam Lallana and Radamel
Falcao wanachukuliwa kama ‘ambidextrous’
kutokana na uwezo mkubwa walionao wawapo uwanjani katika utumiaji wa miguu
yao.Hawa wamezaliwa wakitumia mguu wa kulia kwa ufasaha zaidi na kisha wakajifunza kutumia mguu wa kushoto.Wako wengi lakini hawa ni baadhi yao.
Ukiacha na wachezaji hawa ambao wamejifunza kutumia miguu
dhaifu lakini kuna baadhi ya wachezaji wamezaliwa wakiwa na uwezo wa kutumia
miguu yote kwa ufasaha zaidi, anapopiga mpira kwa kutumia mguu wa kulia na mguu
wa kushoto huwezi kuona tofauti Andreas Brehme, Shinji Kagawa, Paolo Maldini
and Pavel Nedvěd,Toni Kroos, Adriano Correia na Julian Draxler.
Lakini ukiachana
na hawa wote mchezaji ambaye ananistaajabisha zaidi ni Mhispaniola anayekipiga
katika klabu ya Arsenal Santi Carzola huyu ndiye mchezaji pekee mwenye uwezo wa
kutoa pasi,kupiga mashuti ya umbali mrefu na kufunga magoli katika sehemu yoyote ile ya uwanja kwa kutumia miguu yote
100%.Unapomuangalia Santi Carzola lazma uvutiwe na staili anayocheza ,anakuwa
ni hatari na mwiba mkali anapolikaribia lango la mpinzani.Arsene Wenger kocha
wa Arsenal amekuwa akimpanga nafasi yapembeni katika mechi mbalimbali lakini
alimtumia katika sehemu ya kiungo cha kati amahakika aliweza kutumia vyema
uwezo aliokuwa nao na kuinyanyasa timu pinzani vilivyo.
Ama hakika ukianza kuitadhimini kazi ya uumbaji ya Mwenyezi
Mungu lazma upige goti kumsujudu na kumshukuru.Ninashukuru sana kuwa miongoni
mwa ‘ambidextrous’ katika matumizi ya mikono.Mungu amevigawanya vipaji kwa watu
mbalimbali,unaweza ukawa na kipaji Fulani usikigundue changamoto inabaki kwako kufanya kila njia
ukigundue kipaji chako.
Imeandaliwa na.....
Katemi Mugisha Methsela
(C.E.O BantuTz.com)
+255 785 442 107
+255 716 418 657
0 comments:
Post a Comment