Madaktari mjini Devon wanaunga mkono
kampeni mpya inayowaagiza raia kuwatembelea madaktari wao iwapo
wanahisi kuwa na kiungulia kwa siku kadhaa kwa kuwa huenda ikawa ishara
ya ugonjwa wa saratani.
Zaidi ya watu 10,000 hufariki kutokana na
saratani ya tumbo ama ile ya koromeo kila mwaka nchini Uingereza ambayo
ni sawa na watu 28 kila siku.kampeni hiyo inayofanywa na idara ya afya ya uma nchini Uingereza inasema watu sita kati ya kumi hawajui kwamba kiungulia huenda kikawa ishara ya Saratani.
Pia inasema kuwa karibia nusu ya watu hutembelea madaktari wao iwapo wanaugua kiungulia kwa wiki tatu ama zaidi.
Daktari Tom Debenham kutoka Devon na mkuu wa kliniki za kazkazini,mashariki na magharibi mwa Devon anasema kuwa watu wanafaa kuelezwa kuhusu uhusiano kati ya kiungulia na saratani.
''Iwapo unahisi kiungulia kila mara,nenda ukamuone daktari ,hata iwapo unatumia dawa na unahisi zinakusaidia''.
''Huenda si kitu chochote hatari lakini iwapo ni saratani kuigundua mapema inakuwa rahisi kuitibu.'',alisema daktari huyo.
Watu pia wameagizwa kuwatembelea madaktari wao iwapo kila wanapomeza chakula wanahisi kwamba chakula kinazuiliwa katika koromeo.
0 comments:
Post a Comment