Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, 31 January 2015

Msikiti mkubwa Afrika wajengwa Algeria


Msikiti utakaoshindana na maeneo mengine ya Kiislam ya kuabudia makubwa kuliko yote duniani unajengwa katika pwani ya kaskazini mwa Algeria.
Nini malengo ya kujenga msikiti mkubwa kama huu?
Nusu ya eneo katika ghuba ya Algiers, jengo kubwa taratibu limeanza kuibuka kutoka ardhini.
Katika sehemu moja kitakuwa chumba cha kuabudia cha Msikiti Mkuu wa Algiers. Katika sehemu nyingine kutakuwa na mnara mrefu kuliko yote duniani, ukiwa na urefu wa mita 265 kwenda juu.
Kutakuwa na shule ya korani, maktaba na jumba la makumbusho, na maeneo na bustani zenye miti ya matunda mbalimbali.
Wageni watawasili katika magari, matreni na hata maboti. Jengo hilo, litakalokuwa na uwezo wa kuchukua watu 120,000 people, litaunganishwa na bandari katika bahari ya Mediterani katika njia mbili za mandhari ya kutembea.
Msikiti huu utakuwa wa tatu kwa ukubwa wa eneo duniani, kwa mujibu wa wataalam wa majengo na kuwa msikiti mkubwa kuliko yote barani Afrika.
"Ni moja ya miradi ya karne," amesema Ouarda Youcef Khodja, afisa mwandamizi katika wizara ya nyumba na mipango miji, wakati alipotembelea eneo hilo la ujenzi.
Bi Ouarda amesema Rais Abdelaziz Bouteflika alitaka msikiti huo kuwa"Mnara wa Uislam na kwa mashujaa wa mapinduzi ya Algeria" - vita vya kupigania uhuru kutoka Ufaransa.
Lakini pia unaamanisha kuwa ishara kwa siku za baadaye. "Mnara huu utakuwa kitu cha kurejelea katika mapinduzi ya sasa-mapinduzi ya maendeleo ya Algeria."
Kama ilivyo kwa miradi mingine mikubwa, inayofadhiliwa kutokana fedha inayotokana na mafuta, ujenzi wa msikiti huu unategemea wataalam na wafanyakazi kutoka nje. Umebuniwa michoro na wataalam wa majengo wa Ujerumani na unajengwa na kampuni ya ujenzi ya China iitwayo China State Construction Engineering Corporation, ambayo ina mamia ya wafanyakazi wanaoishi katika eneo la ujenzi.
Na kama ilivyo kwa miradi mingine, mradi huu umechelewa kutekelezwa. Wizara ya nyumba na mipango miji hivi karibuni ilichukua jukumu la kusimamia ujenzi wa msikiti huo kutoka wizara ya masuala ya dini. "Mungu akipenda", anasema Bi Youcef Khodja, kwa sasa utakamilika mwishoni mwa mwaka 2016, japo hata hiyo tarehe, ujenzi utakuwa umechelewa kwa zaidi ya mwaka mmoja kutoka muda uliokuwa umepangwa.
Vipimo vya msikiti huo, na eneo lake na gharama yake inakadiriwa kuwa dola za Kimarekani bilioni 1-1.5, ikionyesha kuwa ni kipaumbele cha serikali.
Sababu moja ya kutekelezwa kwa mradi huu ni uungwaji mkono na Bwana Bouteflika ambao utakuwa ukumbusho wa urais wake nchini Algeria.
Sababu nyingine inaweza kuonekana kwa ushindani wa mara kwa mara na majirani zake, Morocco. Msikiti wa Algiers utaupita kidogo msikiti wa Hassan wa Pili ulioko Casablanca kwa ukubwa wa eneo na kwa urefu wa mnara.
Lakini msukumo mkubwa huenda ukawa jaribio la serikali kujenga utambulisho wa taifa kidini na kutangaza Uislam kwa kuweka udhibiti juu ya misikiti na maimam wanaosalisha humo.
Jitihada hiyo iliyoanza pamoja na harakati za uhuru mwaka 1962 na kupata dharura na mgogoro wa kiraia na wapinzani wa Kiislam katika miaka ya 1990, wakati huo serikali ilipoteza udhibiti wa baadhi ya misikiti kwa wahubiri waliochochea upinzani dhidi ya utawala wa serikali.
Ni kwa mantiki hiyo Algeria inajenga msikiti mkubwa wa kisasa, kitu ambacho kilikuwa kinakosekana mpaka sasa - anasema Kamel Chachoua, mtaalam wa Algeria wa masuala ya dini katika Taasisi ya Utafiti na Elimu katika Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislam mjini Marseille.
Uamuzi wa kujenga msikiti huu ulikuwa "ukimaanisha kuwadhibiti wapiganaji wa Kiislam. Ni wazo la kuunda Uislam wa kitaifa baada ya kitisho cha miaka ya 1990 na kuundolea Uislam taswira mbaya na kuufanya kuwa karibu zaidi na serikali na kupambana na misimamo mikali ya kidini."
Msikiti huu una maana ya kuwa ishara muhimu katika sehemu ya Algiers ambayo imeshuhudia vitendo vingi vya misimamo mikali ya kidini katika miaka ya 1990, amesema.
"ni njia ya kuficha misikiti midogo na kuidunisha. Ni namna ya kusema: 'Tunapenda Uislam, lakini Uislama wa kisasa'. "Unaweza kujenga miskiti midogo 1,000 lakini haionekani - haionyeshi kuwa serikali iko katika mchakato wa kuonyesha udhibiti wake juu ya Uislam na kwamba inajivunia Uislam."
Wazo la kuhamasisha utaifa wa dini ya Kiislam ambayo inaondokana na itikadi zenye misimamo mikali kutoka nchi za Ghuba au kwingineko linaonekana katika jitihada za serikali za kutangaza na kushirikisha Sufi zawaya, au sheria za kidini. Pia inajidhihirisha katika utaalam wa ujenzi wa msikiti mpya wa Afrika Kaskazini, wenye mnara mmoja wa muundo wa pembe nne.
Mnara utakwenda juu ya eneo la Mohammedia, na juu ya mabaki ya ukoloni uliopita nchini Algeria. Moja kwa moja nyuma ya eneo la ujenzi ni jengo kubwa lililotumika kukaliwa na wachungaji wa kimisionari kutoka Ufaransa waliojulikana kama "peres blancs, au white fathers". Chini kidogo ya barabara ni eneo la kiwanda cha zamani cha mvinyo.
Msikiti huo umebuniwa kuwa ishara ya utambulisho wa Algeria mpya, lakini utambulisho huo bado unapiganiwa.
Baadhi ya wakosoaji wanauona msikiti huo kuwa zaidi kuwa ishara ya maelewano baada ya mgogoro na wanasiasa waislam kuliko kuwa njia ya kupambana na wasilam wenye misimamo mikali.
"Kipaumbele ni kusema: 'Angalia tulivyo nchi ya Kiislam," anasema Amira Bouraoui, mfuasi wa vuguvugu la upinzani la Barakat. "Ni njia nyingine ya kuwanyamazisha wapinzani wa Kiislam na kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa."
Bi Bouraoui hivi karibuni alitishiwa katika mtadao wa kijamii wa Facebook baada ya kuuliza kama sauti ya vipaza sauti ingeweza kupunguzwa. Wananch iwa Algeria wasiofungamana na dini wanaona hili kama mfululizo wa mifano ya kufuatilia uislam na kukosekana kwa uvumilivu wa kidini.
Hata hivyo kwa kawaida, iwapo Wa-Algeria wanaonekana kuwa watazamaji zaidi, hiyo ni hali ya juu juu, anasema Nacer Djabi, mwana sociolojia katika chuo kikuu cha Algiers. "katika kiwango cha kijamii si fikirii kama wanadini hasa, anasema Djabi.
"Ni watu wasiotaka mabadiliko sana, mabadiliko wanayoonyesha ni ya juu juu. Unaweza kuona hilo katika mitaa ya Algiers - kuna wasichana wengi wenye hijab, lakini hizo haziwazuii kuwa na wapenzi wa kiume, kunywa bia.
"Wa- Algeria wengi, wafanyabiashara, wanakwenda Mecca, wanaswali mara tano kwa siku", anasema."Lakini hali halibadili tabia yao kama wananachi kama Waislam."
Kwa upande wao wakazi wa Mohammedia wanaonekana kutofurahishwa na ujenzi wa msikiti mkubwa katika maeneo yao, wakisema fedha hiyo ingetumika katika mambo mengine.
"Unatakiwa kuanza na elimu na afya, na baadaye unaweza kufikiria kuenzi dini," anasema Racim, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22.
"Katika mtazamo wa Kiislam, mahali pa kuswalia si muhimu sana - ni kile kilichoko moyoni."

Je,kiungulia ni ishara ya saratani?


Madaktari mjini Devon wanaunga mkono kampeni mpya inayowaagiza raia kuwatembelea madaktari wao iwapo wanahisi kuwa na kiungulia kwa siku kadhaa kwa kuwa huenda ikawa ishara ya ugonjwa wa saratani.
Zaidi ya watu 10,000 hufariki kutokana na saratani ya tumbo ama ile ya koromeo kila mwaka nchini Uingereza ambayo ni sawa na watu 28 kila siku.
kampeni hiyo inayofanywa na idara ya afya ya uma nchini Uingereza inasema watu sita kati ya kumi hawajui kwamba kiungulia huenda kikawa ishara ya Saratani.
Pia inasema kuwa karibia nusu ya watu hutembelea madaktari wao iwapo wanaugua kiungulia kwa wiki tatu ama zaidi.
Daktari Tom Debenham kutoka Devon na mkuu wa kliniki za kazkazini,mashariki na magharibi mwa Devon anasema kuwa watu wanafaa kuelezwa kuhusu uhusiano kati ya kiungulia na saratani.
''Iwapo unahisi kiungulia kila mara,nenda ukamuone daktari ,hata iwapo unatumia dawa na unahisi zinakusaidia''.
''Huenda si kitu chochote hatari lakini iwapo ni saratani kuigundua mapema inakuwa rahisi kuitibu.'',alisema daktari huyo.
Watu pia wameagizwa kuwatembelea madaktari wao iwapo kila wanapomeza chakula wanahisi kwamba chakula kinazuiliwa katika koromeo.


Iyanya kutoka Nigeria amem-diss Jaguar wa Kenya kwa kumuita mvivu

iyanay; jaguar 
 
Mbali na wawili hao kufanya collabo ya pamoja kwenye ngoma ya Jaguar mwenyewe iitwayo "One centimeter rmx" akiwa amemshirikisha Iyanya kutoak Nigeria waliingia kwenye utata baada tu ya kutoa ngoma yao hiyo.
 
Utata huo ulianza baaada ya kusambaa kwa video hiyo ambapo Jaguar alitaka ifike kimataifa lakini hakuonesha juhudi zozote za kui-push video hiyo.Iyanya alisema kwamba Jaguar ni mvivu wa kusukuma ngoma zake zifike kimataifa kama wengine wanavyofanya.
Pia alisema hakuona Iyanya nimefanya collaboz na Diamond na Sauti soul laikini wao ndio wanao push ngoma zao kufika vituo mbali mbali lakini kwake Iyanya hafanyi hvyo kwani amekua akitegemea mimi ndio nifanye hivyo.

Mazishi ya baba wa Peter na Paul -P square yanafanyika leo


 
Wasanii waakubwa ambao ni mapachaPeter na Paul maarufu kama P-square kutoka Nigeria  wanataraji kumzika baba yao mzazi  Pa Mosses Okoye leo aliefariki november mwaka jana.
 
Mazishi hayo ambayo yatafanyika ki mila pia yameweza ku make headlines kutokana na kucheleweshwa kuzikwa kwa baba yao huyo.
Mazishi yatafanyika nyumbani kwao Lfite duru Anambra state huko huko nchini Nigeria

Huu ndio muonekano mpya wa Rihanna

Mwana dada mwenye skendo za kila kukicha ame-post picha ikimuonyesha munekano wake wa nywele na hata sura.
 
Muonekano huo unatumika katika jarida moja linalohusu muziki na maisha ya watu maarufu kwa ujumla.Rihanna ndie atakae tumika kama cover photo.


Huu ndio muonekano mpya wa Rihanna

Mwana dada mwenye skendo za kila kukicha ame-post picha ikimuonyesha munekano wake wa nywele na hata sura.
 
Muonekano huo unatumika katika jarida moja linalohusu muziki na maisha ya watu maarufu kwa ujumla.Rihanna ndie atakae tumika kama cover photo.


Huu ndio muonekano mpya wa Rihanna

Mwana dada mwenye skendo za kila kukicha ame-post picha ikimuonyesha munekano wake wa nywele na hata sura.
 
Muonekano huo unatumika katika jarida moja linalohusu muziki na maisha ya watu maarufu kwa ujumla.Rihanna ndie atakae tumika kama cover photo.


Kanye west:"Mimi ni baba bora kwasababu ya Kim Kardashian na mwanangu North West


kanye-on-having-more-kids-710x400-2 
 
Mkali wa rap nchini marekani na baba wa familia Kanye West,aliyasema hayo katika kipindi cha The Ellen Degeneres show ambapo kanye alifunguka ukweli kuhusu yeye na maisha yake paoja na familia yake.
Alikuwa akihojiwa juu ya video yake mpya iitwayo "Only One" ambapo kwenye nyimbo hiyo amezungumzia maisha na familia yake akimtaja mkewe Kim Kardashian pamoja na mwanae North West.

On marriage and family changing him: “I have always someone to think about going home to: something not only to be brave for what I want to do for humanity, but also to be more protective of myself for my family.”
On having a bigger family: “We’re trying,” he said. “I just want whatever Kim wants.”

Mpinzani wa Obama mwaka 2012 ajiondoa kugombea Uchaguzi Marekani.

 
Mitt Romney, mgombea wa chama cha Republican aliyeshindwa na rais Obama katika uchaguzi wa mwaka 2012 ameamua kutowania tena wadhfa huo.
Bwana Romney mwenye umri wa miaka 67 amesema kuwa ameamua ni muhimu kuwapatia viongozi wengine katika chama hicho fursa ya kuchaguliwa kama wagombea.
Taarifa yake inajiri wiki kadhaa baada ya tangazo lake kwamba atawania kwa mara nyengine.
Hatua yake ya kutowania inawapa fursa wafadhili kuwaunga mkono wagombea wengine.
Aliyekuwa Gavana wa jimbo la Florida Jeb Bush ,gavana wa new Jerzy Chris Christie na seneta Rand Paul ni miongoni mwa wale wanaowania kuingia ikulu ya whitehouse.

Apple yavunja rekodi kwa uuzaji wa vifaa vyake duniani.

Kampuni ya kutengeza vifaa vya elektroniki, Apple, imetangaza kupata faida ya dola bilioni 18.8 katika kipindi cha miezi minne ya mwisho mwaka jana , na kuifanya kuwa kampuni ya umma iliyopata faida kubwa zaidi duniani.
Apple bila shaka imeipiku,ExxonMobil iliyopata faida ya dola bilioni 15.9 mwaka 2012 kulingana na ripoti ya kampuni ya Standard and Poor's.

Inaarifiwa hii ndio faida kubwa zaidi katika historia ya kampuni hio kuwahi kushuhudiwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mdadaisi mkuu wa kiuchumi wa kampuni hio, Tim Cook alisema kuwa hitaji la simu za iphone duniani ni kubwa kupindukia.
Hata hivyo, alisema kwamba hitaji la tabiti au iPad haliko juu kama ilivyotarajiwa na liliendelea kushuka kwa asilimia 18 mwaka 2014 ikifananishwa na mwaka 2013.

Kadhalika hitaji la simu ya iPhone 6 Plus lilionekana kuwa chachu katika faida za kampuni hio.
Hata hivyo, Apple haikufafanua mauzo ya simu ya iPhone 6 na simu nyinginezo.
Hisa za kampuni ya Apple zilipanda kwa asilimia 5 baada ya soko la hisa Marekani kufungwa Jumanne.
Mmoja wa wanaofuatilia mauzo ya bidhaa za Apple sokoni, na mhariri wa mtandao wa "Cult of Mac" alisema kwamba mauzo ya iPhone yamekuwa juu sana ikilinganishwa na matarajio.

Diamond Platnumz,Davido na Wizkid wamaliza tofauti zao.

 
Wakali hawa wanaofanya vizuri kwenye ramani ya muziki Africa na kimataifa kwa ujumla hatimae bifu lao limeisha.
Uthibitisho huo wa bifu la wakali hawa watatu limeisha mara baada ya Diamond platnumzna Wiz kid ku-post kwenye page zao za instagram nyimbo mpya ya Davido aliyo mshirikisha Uhuru na Dj bucks.
Diamond nae ali-post katika account yake kwa kuaonesha kum-ssuport Davido kwa nyimbo yake mpya.
 
Hiyo ina thibitisha kuwa bifu baina yao wote limeisha.

Baba ajiua kutokana na picha za mwanawe


Baba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi zamwanawe wa kike katika jarida la Playboy nchini Romania.
Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa 'amepos' katika jarida hilo la Playboy na punde babake alipogundua kuhusu picha hizo, alizongwa na mawazo na hata kumkana mwanawe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, msichana huyo mwenye umbo la kuvutia alisema, '' babangu aliacha kuongea na mimi na kuonekana mwenye hasira sana''.
"alipogundua kuwa picha hizo zilikua zangu, alijitenga sana na kujaribu kunitenga na mimi''.
Nilidhani labda angesahau na sikudhani hata siku moja angejitoa uhai.
 

Mwanamitindo huyo Loredana Chivu mwenye mamia ya picha akiwa nusu uchi kwenye akaunti yake ya Instagram, alikuwa na uhusiano wa karibu sana na babake lakini alisema yote hayo yalibadilika baada ya babake kuona picha zake akiwa nusu uchi.
Alipokwenda kumtembelea babake miezi michache baadaye, baada ya kuamua kwamba kimya kilikuwa kimeendelea kwa muda mrefu sana, alishtuka sana kumpata babake akiwa amejitoa uhai
"nilipata akiwa na kamba shingoni akiwa ananing'inia chumbani''.
Loredana,anayeishi nchini Romania, anasema kuwa tangu kifo cha babake, amekuwa akiwaza na kuwazua kwamba aliamua kujiua kwa sababu ya mgogoro kati yetu na hasa kuhusu picha zangu zilizoziona kwenye jarida la Playboy.
''Najuta sana kwamba hakuwahi kupata muda wa kuzungumza na babangu kuhusu yaliyotokea''.
''Hakuwacha ujumbe wowote kabla ya kujitoa uhai, siku zote tulikuwa na uhusiano mzuri lakini yote yalibadilika baada ya baba kuona picha zangu nikiwa uchi. Bado inaniuma sana na singemtakia mtu yeyote kupatwa na kama yaliyonikuta''.

Sister wa kanisa kubwa duniani ajifungua mtoto wa kiume nchini Italy

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/01/nun_635x250_1390217286.jpg
Sister mmoja huko nchin Italia amejifungua mtoto wa kiume mara baada ya kulalamika kwa muda mrefu kwamba anasumbuliwa na tumbo ndipo kuwaishwa hospitalini na kujifungua mtoto licha ya kuwa alikua anaishi jumuia ya wanawake watupu katika kanisa katoliki Italia.
 
Sister huyo mwenye umri wa miaka 31 anaetokea kikundi cha masister cha Santa Chiara mwenye asiri ya Amerika ya kusini alifikishwa hospitalini hapo na baada ya muda alizimia ndipo madaktari walipoa amua kumpeleka labour na akajifungua.
 tIL9B3Y-360
WAtu wengi wanajiuliza amewezaje kupataujauzito huo ikiwa alikula kiapo cha usafi na utii wa kiroho.kwa lengo la kulitumikia kanisa hilo.
Tukio hili linataka kufanana na tukio la mwaka jana ambapo sister Salvador alipata mimba na kujifungua mtoto wa kiume na kumuita jina la Papa Francis.

Wema sepetu akamatwa na polisi kwa bajaji


 
 
Mwana dada muigizaji wa filamu za kitanzania asie kauka kwenye vichwa vya habari kwenye mitandao na midomoni mwa watu,amefanya tukio jingine la kushangaza jamii kitendo kilicho pelekea mapolisi kuja kumkamata.
Polisi wamejikuta wanapata heka heka ya kumshika mwana dada Wema Sepetu kwa kosa la kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha bila kibali hali iliyo pelekea kuwaudhi jirani zake.
Polisi hao walifika asubuhi ya leo kwa lengo la kumkamata mwana dada huyo asiye ishiwa vimbwanga kila siku,ndipo Wema alipo anzisha vurugu.
 
Wema yeye anavyo dai ni kwamba kulikua na birthday ya rafiki yake aliefahamika kwa jina moja Neema,mmoja wa majirani wa Wema alisema kwamba hua ndio tabia yake ya kufanya sherehe na kufungulia muziki kwa sauti kubwa zaidi kitu ambacho kinasababisha kero kwa majirani zake.
Polisi waliamua kuchukua spika za redio hiyo na kumbeba Neema alie semekana ndie aliyekuwa mwenye sherehe.

Msanii Suge Knight akamatwa kwa mauaji


Polisi nchini Los Angeles inasema kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.
Polisi wanasema kuwa bwana Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
Suge Knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death Row Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa mziki wa rap akiwemo Snoop Dogg na marehemu Tupac Shakur.

BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO JANUARI 31

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz mwaka huu