Thursday, 2 October 2014
Mungu aliumba Dunia,Da Vinci aliijenga Dunia.
Katika dunia ya leo ni wanadamu wengi sana ambao wanakumbukwa kwa matendo yao mbalimbali waliyoyafanya wakiwa hai.Tumefanikiwa kuwakumbuka binadamu mbalimbali ambao waliifanyia dunia mambo makubwa na dunia haitweza kuwasahau hata kama imepita miaka 1000.Isaac Newton,Bendel,Adolph Hitler,Pele,Maradona,Garincha ni baadhi tu wako wengi, lakini hao ni baadhi ya binadamu wanakumbukwa kwa mazuri na mabaya waliyoifanyia dunia.
Adolph Hitler anakumbukwa zaidi na WaIsrael kwa maauaji ya kinyama aliyowafanyia baada ya vita ya kwanza ya dunia huku akiwatuhumu kuwa chanzo cha Ujeruman kushindwa katika vita ya Kwanza ya dunia,Hitler alianzisha vita dhidi ya WaIsrael popote pale walipo kutokana na nguvu kubwa za kijeshi alizonazo.Na hapo baadae aliwaua Wayahudi/Waisrael wapatao milioni 6.
Lakini ukiachana na Adolph Hitler ambae dunia nzima inamchukia kwa unyama na ukatili alioufanya lakini Wajeruman wanamkumbuka na kumuweka katika mioyo yao huku wakimpenda kutokana na kulipigania taifa lao.Adolph Hitler alikuwa na sera aliyoiita "Nationalism" kwa lugha yetu tunaita "Utaifa".
Aliipenda Ujeruman na kuiweka moyoni mwake aliumia sana baada ya ujerumani kushindwa vita ya kwanza ya dunia dhidi ya Uingereza,Urusi na Ufaransa.Alipokuwa hospitali amelazwa kisha akapewa taarifa kwamba Ujerumani imeshindwa vita aliumia sana.Hapo baadae alifanikiwa kuipindua dola iliyokuwa madarakani na kisha kufanikiwa kutawala mwaka 1927 aliijenga Ujerumani ikajengeka,alifanya,Dunia ilimchukia ila Ujerumani ilimpenda.Hadi leo hii Wajerumani wanampenda na kujivika roho ya Hitler katika maisha yao,Mjerumani popote pale anasifika kuwa ni mtu shupavu,mwenye moyo mgumu na mfano mzuri kwenye soka,Bundesliga inasifika kuwa Ligi imara Ulimwenguni.
Duniani kuna mtu aliyewahi kutokea na hakika hatoweza kutokea katika kizazi hiki,wahandisi wa majengo na watu mbalimbali wanaohusika na masuala ya mipango miji,wanasayansi,wanamahesabu,wataalamu wa masula ya anga na nyota hakika watakuwa wanamjua vyema mtu huyu.Anaitwa Leonardo da Vinci.
Leonardo Da Vinci kwanza jina lako limekuja kimaajabu sana,yeye aliitwa Leonardo na kipindi hicho alikuwa hatumii jina la pili,akaamua kutafuta majina mengine,kwanza akapata Da ikiwa na maana mtoto wa kiume kwa lugha ya Kiitaliano,kisha akalitafuta "Vinci" hii ni sehemu aliyozaliwa.Hatimaye akapata jina kamili Leonardo Da Vinci
Leonardo da Vinci ni mwanadamu wa kipekee sana aliyewahi kutokea duniani na inaaminika ndiye mwanadamu aliyekuwa na akili "Genius" kuliko wote duniani alizaliwa mwaka 1452 April 15 huko Italy.nje ya mji wa Wedlock karibu na Kitongaji cha Notary, Piero da Vinci.Ni Muitaliano aliyebobea kwenye masuala ya Uhandisi Majengo "Architect",mahesabu,Muziki,uandishi wa mashairi na vitabu,uchoraji,sayansi ya anga,ugunduzi,utengenezaji na uchoraji wa ramani,sayansi ya mifugo,wanyama,na Binadamu
Leonardo da Vinci anakumbukwa sana kwa juhudi na maarifa yake mbalimbali katika kuijenga Ulaya tunayoiona hivi sasa.Kabla ya kuanza kuchora ramani za miji na majengo mbalimbali barani Ulaya,Da Vinci ndiye aliyechora na kutengeneza mashine inayoruka ambayo hapo baadae wanasayansi walitumia teknolojia hiyo kutengeneza ndege kubwa na za kisasi ambazo zinaweza kuruka zikiwa zimebeba mizigo na binadamu.
Mashine inayoruka iliyobuni Leonardo Da Vinci 1488
Vile vile kutokana na uwezo mkubwa alionao aliweza kutengeneza "Theories" mbalimbali moja wapo ni "PLATE TECTONIC THEORY" wale waliosoma Jiografia wanaelewa namaanisha,hii ni "Theory" inayoelezea mitikisiko ya sehemu za ndani ya dunia/ardhi "Lithosphere" ambayo ndiyo chanzo cha kugawanyika kwa mabara mbalimbali huku akiamini mabara yote yalikuwa kitu kimoja na baada ya "motion and forces" mbalimbali zilizo ndani ya ardhi ikapelekea kuanza kugawanyika kwa mabara hayo na kutokea mabara mbalimbali ambayo tunayaona leo hii.
Vile Da Vinci aliweza kuvumbua mashine mbalimbali za viwandani ambapo hapo baadae teknolojia hiyo ilikuja kutumika katika Mapinduzi ya viwanda Uingereza 1750-1850,vile hata kipindi cha Mapinduzi ya viwanda Barani Ulaya teknolojia hiyo ilitumika.
Hakika Da Vinci ni binadamu ambaye hatasahaulika huko Ulay,Kikubwa alichokifanya Leonardo Da Vinci ni kuijenga Ulaya.
Kama nilivyokueleza Da Vinci alizaliwa na kukulia Italia,mnamo mwaka 1466 akiwa na miaka 14 aliibuka kuwa kinakara katika mambo ya kuchora alipokuwa Elimu ya msingi,na hapo baadae alikwenda kwa Andrea di Cione,ambaye alikuwa na Chuo kikubwa cha masuala ya uchoraji,sehemu ambayo Da Vinci alijifunza vitu vingi hususan mafunzo kwa njia ya maandishi na vitendo.
Kutokana na uwezo mkubwa alionao Da Vinci alijiona ana akili nyingi kuliko Di Cione huku akiwa amechora picha ya Bikra Marium akiwa amembeba Yesu na picho hiyo ndiyo inayotumika hadi hivi sasa kwani hapo baadae ilipelekwa katika makao makuu ya Kanisa la Rome na kupigwa chapa zilizosambaa dunia nzima.Vile vile alichora picha iliyosambazwa katika makanisa yote ya Baptism duniani.
Picha ya kanisa la Baptism iliyochorwa na Da Vinci
Da Vinci alianza kuijenga Ulaya mnamo mwaka 1492 ambapo alianza kwa kubuni michoro mbalimbali ya majengo makubwa ambayo hayajwahi kutokea barani Ulaya,alianza kujizolea umaarufu kwa kujenga jengo likiwa limenakshiwa kwa madini ya Bronze katika maeneo ya kanisa huko Milan.Baada ya ujuzi wake na utaalamu mkubwa alipata tenda ya kubuni,kuchora na kusimamia ujenzi wa Ngome kubwa ya Rome,Rome ilijengwa kwa uimara na ustadi mkubwa.Rome ilijipatia umaarufu mkubwa duniani kote kupitia kazi kubwa iliyofanywa na Da Vinci
Mwanzoni mwa vita vya Pili vya Italia mwaka 1499 baada ya Italy kuvamiwa na majeshi ya Ufaransa,Da Vinci alikimbilia katika mji wa kihistoria wa Venice.Venice ulikuja kuwa mji uliopangika vizuri zaidi barani Ulaya na kuwa kivutio kwa watu mbalimbali,teknolojia aliyoituymia Da Vinci kutengeneza majengo na kubuni ramani za mji wa Venice zilishangaza wengi haswa kutokana na aina ya vitu vigumu alivyotumia katika ujenzi,hali inayopelekea majengo hayo kuendelea kuwepo hadi leo hii.
Baada ya Vita kuisha mnamo mwaka 1502, Da Vanci alichukuliwa na aliyekuwa mtoto wa Papa Alexander VI na kumfanya Da Vinci kuwa "Military Architect and Engineer",mtoto huyo wa Papa alimtembeza Da Vinci huko Cesare Borgia,Casena-Italy.
Alifanikiwa kutengeneza ramani ya mji huo kitu kilichoonekana cha ajabu kwa kipindi hicho.Kupitia ramani hiyo Papa Alexander VI alifanikiwa kubuni na kuendeleza enao hilo na kuwa mfano wa kuigwa Baraani Ulaya,kitu ambacho kilipelekea "kuzitoa udenda" dola na ngome karibia zote za Ulaya.
Ramani ya Mji wa Casena iliyoleta mapinduzi katika sekta mbalimbali Italy baada ya kutengenezwa na Leonardo Da Vinci.
Mnamo 1513 baada ya Papa Leo X kushika hatamu,Da Vinci aliamuriwa kwenda kuishi Belvedere huko Vatican-Rome,ambapo alikutana na rafiki zake,walikuwa na shughuli moja tu kuijenga Vatican iliyo ndani ya Rome.Baada ya kumaliza kuijenga Rome vilivyo na kisha ikasimama kama dola imara duniani ikiongozwa na Pope Leo X.Da Vinci alianza kuwa maarufu barani Ulaya hali iliyopelekea kuheshimika sana.
Ufaransa ikiwa chini ya Mfalme Francis I ilivamia mji wa Milan na kufanikiwa kuutawala mnamo mwa 1515,wakafanikiwa kumtorosha Da Vinci ambaye walimsafirisha hadi Ufaransa na alipewa kila kitu anachokihitaji ili aweze kuijenga Ufaransa huku makazi yake yakiwa ndani ya Ikulu ya kiongozi huyo wa Ufaransa iitwayo Château d'Amboise.Mfalme Fransis I alimwambia Da Vinci kwamba "I want to create France as Mechanical Iron"
Da Vinci aliweza kuijenga Ufaransa ikajengeka,alianza kwa kuchora na kubuni ramani katika miji ya Paris,Lens,Nice,Marsaille,Nantes,Schaux kisha akabuni michoro ya majengo mbalimbali na kusimamia ujenzi wa majengo hayo.
Huyo Da Vinci mtu mashuhuri ambaye Ulaya itamkumbuka kwa kazi yake kubwa aliyoifanya.Da Vinci vilevile aliweza kuandika vitabu mbalimbali vinavyoelezea mambo mbalimabali kuhusiana na Uhandisi wa Majengo "Architecture" na kusambazwa Uingereza,Uturuki,Ottomon Empire,Ujeruman,Urusi na baadae kupelekwa Asia,Amerika na Afrika.
Hakika Da Vinci aliijenga Ulaya,kila kiongozi wa dola barani Ulaya alifanya kila njia aweze kumtorosha Leonardo Da Vinci aweze kubuni michoro ya ramani na majengo makubwa,Vilevile ikumbukwe Da Vinci alikuwa na uwezo wa kubuni vifaa/zana mbalimbali za kivita,hivyo basi viongozi hao walifanya kila waliwezalo waweze kumtorosha ili awasaidie katika ujenzi wa dola zao kuwa imara.
Hii ni baadhi ya michoro ya Leonardo Da Vinci inayotumiwa na madhehebu mbalimbali duniani hivi sasa hususan huko Ufaransa,Italy,Kanisa la Roma na Baptism.
Hii ni baadhi ya michoro iliyochorwa na kuandaliwa katika kitabu cha Da Vinci kilichokuwa kinaelezea Mifumo mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Hakika alikuwa ni mwanadamu wa kipekee na aliyejaaliwa "Gifted human being".Aliandaa kitabu chenye kurasa 13000 kikiwa na michoro pamoja na maandishi "Notes" ambacho baadae kilitumiwa na madaktari mbalimbali duniani huku nakala zake zilisambazwa China,Japan,India,Marekani na baadae kikatafsiriwa katika lugha mbalimbali.
Huyo ndiye Leonardo Da Vinci ambaye huku Afrika hakumbukwi na kutambulika sana kwa sababu kazi zake kubwa alizifanya Ulaya,bara ambalo ama hakika hadi leo ukipata nafasi ya kutembela miji kama Venice,Rome,Paris,Madrid,Lisbon,Munich,Moscow,Marseille utastajaabu uwezo mkubwa aliokuwa nao Da Vinci.Leonardo Da Vinci alifariki May 2, 1519 (akiwa na miaka 67) Amboise,Ufaransa katika mikono ya Mfalme Fransis I ambaye hapo baadae alitoa ushuhuda kwamba Da Vinci kabla ya kifo chake alikwenda katika sala ya toba kanisani.
Leonardo Da Vinci akiwa mikononi mwa Mfalme Fransis I wa Ufaransa wakati wa kifo chake.
Huku dunia ikiendelea kumkumbuka shujaa huyu,imefikia hatua baadhi ya waigizaji wakubwa kuihiza sinema mbalimbali zinazoelezea kipaji chake kama vile Da Vinci Demons.
Ufaransa ni miongoni mwa nchi zilizofaidika na kazi ya Da Vinci,ili kumkumbuka na kumuenzi walitengeneza sanamu ya Leonardo Da Vinci huko Amboise-Paris.
Sanamu ya Leonardo Da Vinci iliyotengenezwa huko Amboise-Paris.
Natumai umejifunza kitu kutoka kwa Leonardo Da Vinci,lakini kizazi hiki sio wote ambao wanamkumbuka na kumtambua mtu huyu aliyejitolea kuijenga dunia baada ya Mungu kuiimba Dunia.Hakuna ramani au jengo lolote lile lililojengwa duniani bila kutumia mawzo "Ideas" za Leonardo Da Vinci.
MUNGU ALIUMBA DUNIA,DA VINCI ALIIJENGA DUNIA.
Mtandao Moya wa kijamii (Social Network) kutoka BantuTz inakuja hivi karibuni.Itakuwa na vitu mbalimbali ya kuvutia,BantuTz imepanga kuleta mageuzi makubwa katika nyanja mbalimbali za maisha kupitia mtandao huo.Kaa mkao wa kula.
Imeandaliwa na.............
Katemi Methsela
0 comments:
Post a Comment