Mwaka 1971 nduli amin aliingia madarakani kama Rais wa Uganda,Alimkuta
tayari Mwalimu Nyerere ameshakuwa Rais wa Tanzania.Licha ya kuwa Nyerere alimtangulia
Iddi Amin kama Rais,Pia Nyerere alikua mkubwa kwa umri kuliko nduli Amin.Lakini
hiyo haikuwa sababu ya Nduli Amin kumuheshimu Nyerere.Nduli hakumuheshimu
Nyerere kwasababu alikuwa akiionea Tanzania na Nyerere vile atakavyo.Mwaka huo
huo wakati anaingia madarakani alijaribu kuvamia Mji magharibi(Kagera),Ingawa
hakufanikiwa lakini bado alifanikiwa kuitesa kidogo Tanzania.
Amin bado akaendelea kumdharau
Nyerere na Tanzania yake,Siku moja alimwandikia barua Mwalimu Katika barua hiyo
Dada alimmwambia Nyerere hivi "Nataka
nikuhakikishie kwamba nakupenda saana, na kama ungelikua mwanamke basi
ningefikiria jinsi ya kukuoa japo kichwa chako kimejaa mvi. Lakini kwakuwa wewe
ni mwanaume basi uwezekano huo haupo". Kwa Kashfa hii Nyerere hakujibu
kitu.Bado Amin akaendelea kutembea kifua mbele huku akiamini Tanzania na
Nyerere si kitu.Mwaka 1978 Iddi Amin alivamia tena Mji magharibi(Kagera),na
kufanikiwa kuuteka Mji,Amin akaendelea kutamba na kusema kuwa alitumia dakika
25 tu kuiteka Kagera.Amin aliendelea
“ na hii bendera imeandikwa chama cha
mupinduzi,lakini mimi nataka nyinyi siku ngine kama maneno itakuwa mbaya nyinyi
mtarudi mtasafisha mpaka Dar-es-salaam”.
Baada ya hayo Nyerere uvumilivu
ukamshinda
“Tunayo
kazi moja Watanzania, tunayo kazi moja tu, ni kumpiga.Uwezo tunao Sababu
tunayo na Nia tunayo.”
Hayo ni maneno ya
Nyerere baada ya kushindwa kuvumilia maneno na mambo ya Amin anayowafanyia
Watanzania.Nyerere akafanikiwa kuiongoza Tanzania kumpiga Amin,Tangu Kupigwa
kwake na Nyerere Amin hakusikika tena anaizungumzia Tanzania wala
Nyerere.Alimuheshimu Nyerere Baada tu ya Kumpiga.
Yaliyomkuta Nyerere kwa Amin ni kama kesi ya Wenger kwa Mourinho.Licha ya Wenger kumzidi
Mourinho umri na muda wa kazi lakini Mourinho hamuheshimu wenger hata
kidogo.Mourinho anamdharau Wenger kwasababu
kila siku akikutana naye anamfunga,Mpaka sasa ameshamfunga mechi 7 kati
ya 12 walizokutana,Tangu Mourinho arejee nchini uingereza kikosi cha Arsene Wenger akijafunga hata goli moja kwenye
lango la Chelsea,Mechi 4 za mwisho Chelsea chini ya Mourinho imeshaifunga
Arsena bao 10 huku Arsenal hawajafunga hata goli moja.Unafikiri Mourinho
ataanzaje kumuheshimu Wenger?.Kama kila siku akikutana naye anampa kipigo cha
uhakika kwanini asitembee kifua mbele dhidi
ya wenger?.Hata mimi ningekuwa Mourinho ningekuwa nina kila sababu ya
kumuita Wenger ‘Specialist in Failure’
Wenger uwezo wa kufuta aibu anayoipata kutoka kwa Chelsea na Mourinho anao,Sababu ya kuwa juu
ya Chelsea anayo ila anaonekana hana nia tu.Ukiangali Chelsea na Arsenal
utagundua ni klabu mbili tofauti.Kwa Uingereza
ukiacha Manchester United hakuna timu nyingine yeyote inayoifikia Arsenal
Kiutajiri.Arsenal ina uwezo mkubwa wa kutumia kuliko Chelsea,Lakini leo hii
ukiangalia Kikosi cha Chelsea huwezi
kufananisha na cha Arsenal hasilani.Chelsea wana kikosi kilichoshiba.Arsenal
kwa utajiri walionao ilibidi wawe na kikosi kizuri zaidi ya Chelsea,Lakini
haipo hivyo.Hiyo yote ni kutokana na sera mbovu za usajiri za Arsene Wenger.Sera
za Wenger ndio zinamponza kila siku kupigwa na kunyanyasika na timu zinazofanya
usajiri mzuri kuliko yeye.
Mourinho
ana Costa Wenger ana Welbeck,Kati ana Matic wakati wenger ana Flamin,Hiyo ndio tofauti yao huo ndio ujinga unaomfanya Wenger
aendelee kuwa ‘kubwa jinga’kwa Mourinho.Wenger hana ujanja zaidi ya kutumia
pesa nyingi kuwaleta wakina khedira na Cavani kama kweli ana nia ya kuondokana
na aibu anayopata kila siku kutoka kwa Mou.
Wengi
watapinga na kuniambia wenger hana sababu ya kufanya usajili kwa ajili ya
kumfunga Mou tu,Hapo Mou nimemtolea mfano tu.Maana yangu kubwa Ni kuwa
Wenger lazima afanye usajiri wa Nguvu
ili aweze kushindana na timu nyingine kubwa zenye kaliba ya Arsenal kama Bayern,United,Madrid na Barcelona.Timu
hizo nne ukijumlisha na Arsenal ndio timu 5 Tajiri Duniani lakini timu nne ni
tofauti kabisa na Arsenal ndani ya uwanja.
Wenger
inabidi awe na nia ya dhati kama Nyerere ya kuondoka kwenye utumwa wa kuonewa na nduli
iddi Amin. Wenger Uwezo anao,Sababu anayo ila hana budi kubadilishe nia yake kwa kuanza kutumia utajiri wa arsenal ipasavyo
ili aende sawa na wapinzani wake.Wenger kama anataka heshima yake irudi ni
lazima aanze tena kuwaadabisha wapinzani wake.Ferguson alikua akimuheshimu
Wenger kwasababu alikua akimchapa.Ndani ya miaka 10 ya kwanza ya Arsene
wenger ndani ya Arsenal alikua amemfunga
mechi nyingi Fergi kuliko Fergi alivyomfunga yeye.Hiyo ilikua sababu tosha ya
Fergi kumuheshimu.Lakini mou hatamuheshimu wenger mpaka pale atakapomchapa.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kusoma makala mbalimbali zilizoandikwa na waandishi makini wanaofuata weleni katika uandishi.Bantu Inc iko katika mchakato wa kufungua Social Network kubwa na ya kisasa "Kaa Mkao wa Kula".
Imeandaliwa na.....................
Allen kaijage
0655106767
Kaijagejr@gmail.com
0 comments:
Post a Comment