Kamishna wa Elimu nchini ameifunga kwa mwezi mmoja shule ya sekondari Njombe (NJOSS) baada ya wanafunzi wa shule hiyo kufanya fujo na kuchoma moto shule yao pamoja na shule ya msingi iliyojirani ya shule yao.
Chanzo cha vurugu hizo ni kitendo cha Bodi ya Shule hiyo kuwasimamisha shule wanafunzi wenzao ambao walihusika na kosa la kutoroka shule na kwenda ukumbi wa disko kwenye chuo cha Elimu ya Ufundi kilichojirani na shule hiyo.
Katika kupinga uamuzi huo a wenzao kusimamishwa ndipo wanafunzi hao walifanya fujo na kuchoma moto shule yao na ya msingi iliyojirani. Hasara inakadiriwa kufikia Tsh 100 milioni.
0 comments:
Post a Comment