Mhudumu mmoja wa bustani ya kuhifadhi wanyama ameuawa na chui mwenye milia huko Hamilton New Zealand.
Kupitia kwa kwa mtandao wao wa twitter bustani hiyo ya kuhifadhi ya wanyama ya Hamilton ilisema kuwa
''Tunasikitika kuwa tumempoteza mmoja wa wahudumu wetu wa bustani ya wanyama baada ya kushambuliwa na chui mwenye milia kutoka Sumatra.''
''kwa sasa tunaendelea kutoa msaada wetu kwa familia ya mhasiriwa.
Afisa mkuu wa bustani hiyo bi Juliet Burgess amesikitishwa sana na tukio hilo.
''ni tukio la kuhuzunisha sana kupoteza maisha katika bustani hii''
''Hata hivyo ni mapema sana kuelezea nini kilichotokea hasa lakini uchunguzi wa kina unaendelea'' alisema Sajini Juliet Burgess
Mwanamke huyo alivamiwa na mnyama huyo alipokuwa ameingia kwenye eneo anakoishi ilikuisafisha kwa mujibu wa duru za habari nchini humo.
Bustani hiyo ya wanyama sasa imefungwa huku uchunguzi ukianzishwa kubaini kilichotokea.
Hadi sasa haijabainika iwapo bustani hiyo ambayo imefungwa kwa muda itachukua hatua zipi ima ni kumpiga risasi mnyama huyo ama l.
Hii si mara ya kwanza kwa wahudumu wa bustani ya wanyama kukumbwa na msiba kama huu.
Mwaka wa 2012 mwanamke mwengine aliuawa na tembo katika bustani ya Frankline kusini mwa Auckland nchini humo humo.
0 comments:
Post a Comment