Tuesday, 22 September 2015
NEC: Kauli ya Bulembo ni ya kawaida kipindi hichi cha Kampeni
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeyapuuzia malalamiko kutoka muungano wa Vyama vya upinzani(UKAWA) kuhusu kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdallah Bulembo kuwa “CCM haitafanya makosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani”
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amesema kwa sasa kila chama kiko kwenye kampeni kutafuta ushindi, kwa hiyo kuna baahi ya kauli zitatolewa kama mbinu ya kutafuta ushindi.
Mwisho wa wiki Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliikosoa kauli ya Bulembo, akasema kauli hiyo inaonyesha CCM hawataki kuachia madaraka kwa amani. Mbowe aliilalamikia NEC kwa ukimya wakati kauli kama hizo za kichochezi zinatolewa
Akijibu kauli a Mbowe Lubuva amesema kama kauli ya Bulembo ingekuwa ni 'hatutakubali matokeo' tume ingeingilia kwa sababu NEC imeshasema kuwa kila chama kikubali matokeo.
Lubuva akaongezea na kusema mpaka sasa tume haina chochote cha kusema kuhusu kauli ya Bulembo kwa sababu wameichukulia kama kauli ya kawaida ya kikampeni.
0 comments:
Post a Comment