Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena Nyambabe azungumza juu ya Chadema kuteka Umoja wa UKAWA na kufanya ubabe katika katika upataji wa majimbo na kuacha vyama vingine vilivyo katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam hivi sasa.
Hatua waliochukua wamesema hawatajiuzulu lakini wanasema wataendelea kupambana ndani ya NCCR-MAGEUZI na katika umoja huo watapambana bila UKAWA.
Viongozi waandamizi wa NCCR Mageuzi waliokuwa katika mkutano huo ni Bi Leticia Mosore (Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi –Taifa), Ndugu Mosena Nyambabe (Katibu Mkuu NCCR Mageuzi – Taifa) na Wajumbe mbalimbali wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya NCCR Mageuzi cha NCCR Mageuzi
Hoja kubwa katika mkutano huo ni:-
1.Kushindwa kukubaliana katika mambo mbalimbali waliokwisha kubaliana.
2.Kushindwa kufuata kwa taratibu ya kumpata mgombea wa ukawa.
3. Hakuna kiongozi wa NCCR MAGEUZI tofauti NA Mbatia anayeshilikishwa wala kusikilizwa katika kampeni.
4.Chadema ni UKAWA BARA NA CUF ni UKAWA ZANZIBAR
Endelea kufuatilia kila kitakachokuwa kinajiri kupitia www.bantuz.com
0 comments:
Post a Comment