Watu karibu 4,000 wameondolewa kutoka jela ya Pollsmoor nchini Afrika Kusini baada ya panya wengi kuvamia gereza hilo na kusababisha kifo cha mfungwa mmoja.
Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi kufungwa katika gereza hilo.
"Tumekuwa tukipuliza dawa, lakini kwa sasa, tumelazimika kuwahamisha wafungwa, na itatuchukua siku kadha,” msemaji wa jela hiyo Manelisi Wolela amesema.
Panya hao wameeneza maradhi yajulikanayo kama leptospirosis, yanayosambazwa kupitia mkojo wa wanyama hao waharibifu.
Muungano wa kutetea haki za maafisa wa polisi na maafisa wa magereza umesema gereza hilo lilikuwa limejaa kupindukia na hali ni ya “kinyama”.
Bw Mandela alihamishwa kutoka jela ya Robben Island na kupelekwa Pollsmoor mwaka 1982
Maafisa wa afya wanasema hakuna mtu afaaye kurejeshwa kwenye gereza hilo hadi panya wote waangamizwe.
0 comments:
Post a Comment