Facebook

Tuesday, 22 September 2015

Wanasayansi watengeneza figo maabara.

Je una matatizo ya figo ?
Ikiwa jibu lako ni ndiyo kuwa na subira, maanake hivi karibuni figo zilizoundwa kwenye viwanda na maabara vitakuwepo kuwasaidia.
Nafahamu kuwa waganga wengi wamewaahidi tiba lakini hii sio hekaya tu za abuanuasi la.
Ni ukweli mtupu .
Wanasayansi wanakaribia kuunda figo zitakazo pandikizwa kwenye miili ya wagonjwa na watu wenye matatizo ya figo.
Kauli hii imetangazwa baada ya wanasayansi kuandikisha ufanisi mkubwa katika majaribio ya figo hizo kwa wanyama
 
Figo hizo bandia zilifanya kazi vyema katika nguruwe na panya.
Madaktari hao watafiti wanasema kuwa wanyama hao waliopandikizwa figo hizo walitekeleza majukumu yao ya kawaida ya kibayolojia kama vile kupitisha mkojo kama wanyama wowote wale.
Hilo ndilo lililokuwa kikwazo kikubwa katika majaribio ya awali.
Watafiti hao kutoka Japan waliepuka matatizo ya awali yaliyolemaza majaribio kama haya kwa kukuza vimelea ndani ya figo hizo ilikuzuwezesha vifo hizo bandia kuchunga mkojo na kupitisha pasi na kulowa.
Japo majaribio kwa binadamu hayajaidhinishwa,bila shaka matokeo haya mapya yanatoa muamko mpya katika jitihada za kuunda viungo muhimu vya mwili katika maabara ilikusaidia wagonjwa .


Hata hivyo Viungo vya mwili vinavyoundwa kutokana na sehemu za seli shina za mwanadamu vinategemewa kusuluhisha uhaba wa viungo halisi vya kupandikiza kwa wagonjwa.
Daktari Takashi Yokoo na wenzake katika chuo kikuu cha utabibu cha Jikei kilichoko Tokyo walitumia mbinu hiyo kukuza figo hiyo bandia.
Aidha kikosi hicho kilifurahishwa na matokeo ya figo hiyo bandia zaidi ya wiki 8 baadaye walipowapima panya hao na hata wakajaribu mbinu hiyo ya kipekee kwa mnyama mkubwa zaidi yaani nguruwe ambayo matokeo yake pia yalikuwa sawa na yale ya kwanza.
Profesa Chris Mason, ambaye ni mtaalamu wa maswala ya seli shina na muhadhiri katika chuo kikuu cha London, amefurahishwa sana na matokeoa haya.
''Hili ni tukio la kutia moyo sana.''
''Hata hivyo hili halimaanishi kuwa mbinu hii ya kukuza viungo itafaulu kwa binadamu.'
''Aidha kukuzwa kwa figo kunasaidia kubaini jinsi mwili unavyoondoa uchafu mwilini na ukiangalia wagonjwa wanaolazimika
'kutumia mashini ilikusafisha damu ''dialysis''mbinu hii bila shaka inatoa matumaini makubwa mno''. alisema Profesa Mason.
Watafiti wengine tayari wanafikiria kuhusu mbinu ya kukuza figo,moyo na hata mapafu.
Professa Harald Ott na wenzake wameanza kujaribu mbinu mbadala inayokuza seli shina kutoka kwa viungo vya wazee na kukuza viungo changa.

0 comments:

Post a Comment