NINACHOKIAMINI MAESTRO.
TIMU ZA UINGEREZA NA BALAA LA MASHINDANO YA KLABU BINGWA ULAYA.
Miaka kadhaa nyuma timu za Uingereza zilisha kasi kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya. Lakini hivi sasa imekuwa kinyume chake. Kwa nini timu za Uingereza zimekuwa nyepesi sana kwenye mashindano hayo Ulaya!!?
VIWANGO,WACHEZAJI NA FEDHA.
Viwango vya timu za Uingereza kwa miaka hii ya karibuni havijatofautiana sana. Imekuwa ni jambo la kawaida timu za daraja la chini au za kiwango cha kawaida kuzifunga au kuzisumbua timu zenye viwango vya juu. Hii ni kutokana na miaka ya sasa kila timu ina uwezo wa kupata fedha na kununua wachezaji wanaowataka. Zamani timu kama Manchester United,Liverpool,Arsenal nk ndio zilikuwa na uwezo wa kutamba kifedha lakini sasa wadhamini ni wengi na wanawekeza popote pale kwenye masilahi,hasa mchezo wa soka umekuwa ni biashara kubwa sana kwa miaka ya sasa.
WAPINZANI NA VIWANGO VYAO:
Mashindano ya Ulaya huwa inazikutanisha timu nyingi sana kutoka ligi mbalimbali kutoka kwenye bara hilo. Wachezaji wengi wa sasa wa timu za Uingereza wana viwango vya kawaida kulinganisha na wapinzani wanao kwenda kukutana nao. Mfano ni timu zote ambazo zinawakilisha Uingereza kwenye mashindano ya Ulaya wachezaji wake hawakaribiani hata kidogo kwa uwezo na wachezaji wa timu wanazokutana nazo. Timu hizo sasa wanawategemea wakina Martial,Depay,Herrera,Smalling,McNair,Conquelin,Berlin,Sterling,Bony,Paulista nk ndio wakapambane na timu zenye Lewandowski,Messi,Neymar, Suarez,Chiellini,Vidal, nk . Kama Newcastle, Crystal Palace,West Ham zinawasumbua vilivyo timu tegemezi inawezekana vipi timu hizo zikatoka salama nje ya nyumbani kwao ambako kuna wakina Bayern Munich,Barcelona, Real Madrid,Atletico Madrid,PSG nk wenye wachezaji wa viwango vya ubora wa juu!!?
Wachezaji wa zamani wa timu za Uingereza hawakaribiani wala kulingana kwa viwango na wachezaji wa sasa wa timu hizo. Kama maisha yataendelea kuwa hivyo kwa timu za Uingereza itakuwa ngumu sana kwa timu hizo kupata mafanikio na heshima nje ya ardhi yao.
IMEANDALIWA: Ayo's Mata Maestro
0 comments:
Post a Comment