Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo kwa kushuhudia viwanja vinne vikiwaka moto, ambapo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam, mabingwa watetezi Yanga wamepata ushindi wa tatu mfululizo kwa kuichapa JKT Ruvu mabao 4-1.
Mabao ya Yanga yametiwa wavuni na Donald Ngoma dakika ya 33, Amis Tambwe dakika ya 48, na 60, na Thaaban Kamusoko dakika ya 87.
Kabla ya mchezo huu, mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu hiyo Jerry Muro alitamba kuwa ushindi wa mechi ya leo utakuwa ni salamu kwa "wale wa mchangani" akimaanisha Simba, ambao wanataraji kukutana nao Jumamosi Ijayo ya Septemba 26.
Matokeo mengine katika michezo ya leo, African Sports wamepoteza mchezo wa tatu mfululizo kwa kupigwa mabao 2-0 na Stand United, mabao yote yakifungwa na mchezaji wa zamani wa Simba Elius Maguli.
Mkoani Tanga Mgambo Shooting imeizamisha Majimaji kwa kuichapa bao 1-0 lililofungwa na Fully Maganga dakika ya 24.
Katika dimba la Sokoine jijini Mbeya, palikuwa na Mbeya Derby ikiwakutanisha Mbeya City na Tanzania Prisons, ambapo imeshuhudiwa Mbeya City wakinyolewa kwa kuchapwa bao 1-0 na Tanzania Prisons kwa bao la Jumanne Elifadhili lililopatikana dakika ya 35.
Ligi hiyo inaendelea leo kwa michezo minne kama ifuatavyo.
Coastal Union Vs Toto Africa
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Mwadui Vs Azam FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Nini maoni yako???
0 comments:
Post a Comment