Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima
amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu
dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es
Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akiongea kabla ya kuhojiwa na polisi Mchungaji Gwajima amejitetea
kuwa alichofanya ni kutumia fursa ya kumuonya kiongozi mwenzake
wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake katika makubaliano
waliofikia katika tamko la kuipigia kura ya hapana Katiba
inayopendekezwa.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani
Kardinali Pengo.
Inadaiwa matusi hayo yameonekana kupitia
mitandao mbalimbali ya kijamii ya WhatsApp na mingineyo, ambapo
kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji
Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali
Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.
0 comments:
Post a Comment