Facebook

Sunday, 15 March 2015

Uchambuzi wa Mechi Kali za Leo Ligi Kuu Uingereza na Hispania na Mr.CHOI (KWA TAARIFA YAKO).

CHELSEA vs SOUTHAMPTON
   Tukianzia pale darajani baada ya matokeo City hivi sasa Chelsea watahitaji kushinda mchezo huu pamoja na ule wa kiporo dhidi ya Leicester ili kuweka gepu la pointi 11 na Man City walio nafasi ya pili.
    Katika mchezo wa awamu ya kwanza timu hizi zilitoa sarw ya 1-1 Mane alikuwa mfungaji kwa Soton huku Hazard akifunga kwa upande wa Chelsea.
   Soton ni miongoni mwa timu zenye safu nzuri ya ulinzi pia kiungo kinacho ongozwa na Wanyama,Schnelderlin ambapo kwenye mchezo wa awamu ya kwanza walionesha uwezo mzuri mbele ya viungo bora wa Chelsea wanao ongozwa na Matic anaerejea uwanjani baada ya kufungiwa michezo miwili.
   Watamkosa Mayuka na Rodriiguez lakini urejeo wa beki wa Ubeligiji Alderweireld ambae aliumia kwenye mchezo dhidi ya Man Utd uta amsha hali katika safu ya ulinzi.
   Kasi ya Mane inaweza kuwa chachu nzuri ya vijana wa Koeman kuibuka na point leo pia pengine Pellé ambae mara ya mwisho kufunga ni mwaka jana mwezi wa 12 dhidu ya Everton.
   Upande wa Chelsea licha ya majeruhi ya Mikel Obi ila kikosi hakito kuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na kile kilicho cheza na Psg, kikubwa ni umakini hasa upande wa mipira iliyokufa pia umakini hasa kwa Mane.
   Historia inawabeba Chelsea kwani katika michezo kumi na moja wameshinda mara 6 sare 4 na kupoteza mchezo 1.
   Soton wapo nafasi ya 7 wakiwa na pointi 49 hivyo kiu yao kubwa ni kuwa ktk timu nne bora kitu ambacho kitapelekea mchezo kuwa mgumu.

-----------------------------------------
MAN UTD vs TOTTENHAM
   Katika dimba la Old Trafford wakiwa nafasi ya 4 kwa pointi 53 Man Utd wata wakaribisha Spurs walio nafasi ya 6 kwa pointi 53.
   Ndani ya michezo mitano iliopita dhidi ya Spurs, Man Utd wametoa sare 3 na kufungwa michezo 2 huku matokeo ya mwisho yakiwa sare ya 0-0.
    Halina ubishi kuwa kwa hivi sasa Spurs wapo katika kiwango bora kabisa kikichagizwa na mshambuliaji hatari mwenye magoli 16 akiwa nyuma ya goli 1 kwa wanaongoza Costa na Aguero wenye 17 si mwingine ni Kane.
    Pengine hii leo Man Utd wasipo kuwa makini naye watajikuta wakiruhusu magoli mengi.
   Magoli kipa wa pande zote ni wazuri sana na unapo taja makipa bora wa 5 huwezi kumuacha De Gea na Lloris katika safu za mabeki timu zote hazina tofauti sana kitakwimu.
   Mchezo utakuwa wa kasi sana kulingana na msimamo ulivyo pia aina ya mifumo kwa timu hizi na wachezaji waliokuwa nao.
   Gaal atashambulia zaidi kupitia pembeni kama kawaida yake pia Pochettino staili yake ni ileile ya kushambulia zaidi kuliko kujilinda.
 
-----------------------------------------

  REAL MADRID vs LEVANTE

     Baada ya kupoteza dhidi ya Bilbao na kupelekea wapinzani wao Barcelona kuongoza La-Liga Real watashuka kucheza na Levante walio nafasi ya 17 kwa pointi 25 .
     Real hawajawa na safu nzuri ya ulinzi tangu kuumia kwa Ramos kwa ktk michezo ambayo Pepe amesimama na Varane wamefanya makosa mengi ya kizembe na hata kupelekea timu yao kupata matokeo mabaya.
   Modriç tunataraji ata anza ktk kikosi cha kwanza leo akiwa na Kroos huku Marcelo akirejea na huenda Ramos akacheza.
   Vijana wa Alcaraza Levante hawana matokeo mazuri pindi wakikutana na Real hivyo mchezo wa leo utakuwa mgumu sana kwani wanacheza na Real wanao hitaji matokeo kuelekea mechi ya jadi dhidi ya Barca.
    Uche na Barral wataongoza katika upande wa mashambulizi huku Garcia na Camarasa wakicheza kama viungo tahadhari yao itakuwa kwa safu ya ushambuliaji ya Real ambapo mpaka sasa hawana takwimu nzuri za ufungaji ukifananisha na ile ya wapinzani wao Barca humu Bale akitizamwa sana kutokana na uwezo mdogo kwa hivi sasa anao onesha na mara ya mwisho kufunga ilikuwa mwezi wa kwanza dhidi ya Cordoba.

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment