Wednesday, 4 March 2015
UCHAMBUZI WA MECHI ZOTE ZA LEO LIGI KUU UINGEREZA NA Mr.CHOI (KWA TAARIFA YAKO)
N'CASTLE vs MAN UNITED
Katika dimba la Direct Sports kocha John Carver atahitaji kushinda mfululizo kwa mara ya kwanza baada ya matokeo mazuri aliyo yapata dhidi ya A.villa.
Licha ya kuwa ni miongoni mwa timu zenye wachezaji wengi majeruhi lakini hawajawa na matokeo mabaya sana ukilinganisha na timu kama Everton.
Perez pamoja na Cissé tutaraji kuwaona katika safu ya ushambuliaji huku Ameobi na Gouffran wakitokea pembeni.
Vijana wa Gaal ambao wametoka kushinda dhidi ya Sunderland huku tukishuhudia kiwango kibovu cha Di Maria katika mchezo uliyopita Herrera alicheza vyema sana pamoja na Blind katika kiungo hivyo kazi watakuwa nayo mbele ya Sissoko na Abeid.
N'castle wamekuwa hawatabiriki na mara nyingi wamekuwa wakicheza vyema zaidi pindi wakianza kufungwa, safu yao ya ulinzi imekuwa inakatika sana hasa kwa upande wa Williamson anaecheza na Coloccini.
Man Utd bado hawajawa na kasi kubwa na umiliki wa mpira kwa asilimia kubwa hawana tofauti na wapinzani wao na katika mchezo huu watahitaji point 3 ilikuwa na matumaini ya kurejea Uefa.
NB:: Rooney amefunga mara 12 mbele ya N'castle
Katika michezo 24 ya ligi N'castle wameshinda mara 2 wakitoa sare 5 na kufungwa 17
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
W.HAM vs CHELSEA
Baada ya kupoteza mbele ya C.Palace pale upton park vijana wa Big Sam watatupa karata yao mbele ya mabingwa wa Capital one vinara wa Ligi Chelsea.
W.ham katika michezo 10 wameshinda mchezo 1 na kutoa sare michezo 5 na kufungwa michezo 4 bado kikosi cha Big Sam kinaelekea kuchoka kutokana na nguvu kubwa walizo tumia mwanzoni mwa ligi lakini pia kwa hivi sasa kimekosa mbinu mbadala ya kutafuta ushindi.
Katika safu ya kiungo ambayo inaongozwa na Song pamoja na Noble asilimia kubwa wamekuwa wakitumia nguvu sana kuliko kuucheza mpira kitu ambacho hupelekea kupotezwa kama ikikutana na timu inayo chezea mpira kwa spidi, Safu ya ushambuliaji kina Sakho na Valencia licha ya kufanya vyema ila na yenyewe kwa hivi sasa makali yao yamepungua na katika mchezo wa leo watahitaji kufuta ukame wa W.ham kutokufunga goli dhidi ya Chelsea katika michezo 5 kati ya 6 ya hivi karibuni.
Nene pengine akaanza katika mchezo huu baada ya kuanzia benchi katika mchezo uliopita huku Big sam akiendelea kumkosa Amalfitano aliefungiwa.
Mourinho katika mchezo huu ambao atamkosa Matic huku Mikel akiwa majeruhi pengine atawaduwaza watu wengi kwa maranyingine kwa kumpanga Zouma kama kiungo wa chini kutokana na kutokuwepo kwa Matic na Mikel, licha ya Zouma kutokuwa mzuri katika umiliki wa mpira ila atakuwa msaada kutokana na aina ya viungo wa Hammers wanao tumia nguvu zaidi.
Cuardado bado hatujaona kipya chake pale darajani hivyo ukiondoa katika eneo la kiungo kikosi cha Mourinho kitakuwa kilekile.
NB::
Katika michezo 17 Hammers wameshinda mchezo 1 dhidi ya Chelsea huku wakitoa sare 3 na kupoteza 13.
Mourinho hajafungwa na W.ham katika michezo 7 huku akitoa sare mchezo 1.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
QPR vs ARSENAL
Loftus Road tutashuhudia London Derby kati ya vijana wa Ramsey mbele ya Arsenal.
Qpr wakiwa katika harakati za kuepuka kushuka daraja faraja yao ni kurejea kwa Sadro kuungana na safu ya kiungo iliyo na Isla pamoja na Onuoha,Kranjacar akiwa muhimili wa timu hiyo pamoja na Austin mshambuliaji mwenye magoli 14 mpaka sasa.
Arsenal walionyuma kwa pointi 4 dhidi ya Man City wamekuwa wazuri pindi wakishambulia lakini upande wa safu ya ulinzi hasa kiungo cha chini bado imekuwa ni tatizo kwa kikosi cha Wenger, Sanchez kiwango kimeshuka pia Chamberlain na katika mchezo wa leo watahitaji kufanya kazi ya ziada kutokana na safu ya kiungo cha chini ya Qpr.
NB:: Qpr wameshinda mara 1 kati ya 7 dhidi ya Arsenal katika ligi huku wakifungwa mara 5 sare 1.
Arsenal wameshinda mara 1 kati ya michezo 6 ndani ya dimba la Loftus wakitoa sare 3 na kupoteza 1.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
LIVERPOOL vs BURNLEY
Wakiwa wamecheza michezo 15 mpaka sasa Liver wamepoteza mchezo 1 vijana wa Rogers ambao wamezidi kuongeza wigo wa kucheza Uefa msimu ujao hasa baada ya kuwafunga Man City.
Licha ya kumkosa Gerrald katika michezo kadhaa ila safu ya kiungo imetengemaa ikiongozwa na Henderson ambaye amekuwa na kiwango bora kabisa huku wakionekana kucheza vyema zaidi dhidi ya Man City timu ambayo inaviungo bora kabisa katika ligi.
Licha ya kutochezesha mshambuliaji halisia huku akimtumia zaidi Sterling bado Liver wanasafu nzuri ukilinganisha na wapinzani wao Burnley.
Kwa upande wa Sean Dyche ambaye asilimia 99 ya wachezaji wake ni raia wa Uingereza huku asilimia 1 wakia raia wa Scotland amekuwa hana matokeo mazuri na mchezo ambao walitaraji fanya vyema wa Swansea tukashuhudia Trippier akijifunga na kuipa pointi Swansea, wamekuwa wazuri katika dakika za mwanzo wa mchezo na mwishoni hawana takwimu za moja kwa moja nzuri ndani ya muda wote wa mchezo.
Wakiwa na viungo kama Kightly watakuwa na kazi ya ziada kuwasimamisha Liver ilikujipa matumaini ya kubaki ligi kuu,safu ya ushambuliaji pia imekuwa haina makali ikiongonzwa na Ings.
NB:: Liver wameshinda katika michezo 7 waliocheza na Burnley katika mashindano tofauti pale Anfield.
Burnley hawajafunga goli katika michezo 5 dhidi ya Liver.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
MAN CITY vs LEICESTER
Etihad tutashuhudia Man City walio katika matokeo mabaya kwa hivi huku ndoto za kutete ubingwa wao zikififia wata cheza dhidi ya vijana wa Nigel Pearson walio mkiani mwa Ligi.
Kiwango kibovu alicho onesha Yahaya Toure katika mchezo wa Liver na kuigharimu timu yake, Leo itabidi afanye kazi ya ziada ili kuonesha umuhimu wake pale City tangu arejee kutoka Afcon.
Bony bado hajapata nafasi ya kuanza kati ya michezo 3 aliyocheza mpaka sasa na katika mchezo wa leo dhidi ya timu yenye presha ya kushuka daraja itakuwa vyema kama atacheza na Aguero kuliko Dzeko kuanza maana si mpambanaji.
Kwa hivi sasa mfumo ni 4-4-2 kwa maana hiyo Pellegrin anauwezo wa kumchezesha Toure na Fernandinho huku Milner na Silva wakitokea pembeni na mbele akamuweka Bonny na Aguero.
Pearson atashambulia zaidi kwa kushtukiza kama ilivyo kuwa katika mchezo dhidi ya Everton walio toka sare ya 2-2 huku Cambiasso akicheza vyema.
NB:: Katika michezo 3 ya Ligi ugenini Leicester wameshinda mbele ya City na kutoruhusu wavu wao kuguswa.
Ni mechi 4 tu Leicester hawajaruhusu goli ikiwa ndo kiwango cha chini zaidi msimu huu wa ligi.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa uchambuzi makini katika masuala mbalimbali hususan michezo.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Imeandaliwa na................
Mr CHOI
Choikangta.ckt@gmail.com
WhatsApp -0765 691418
0 comments:
Post a Comment