DORTMUND vs JUVENTUS
1 - 2
Tukianzia pale Westfalenstadion vijana wa Klopp watapambana dhidi ya kibibi kizee cha Turin Juventus iliyochini ya Allegri.
Sare itawawezesha Juve kufudhu hatua ya robo fainal huku ushindi wa goli 1 kwa bila utaifanya Dortmund kutinga robo fainal na kuwa timu ya pili baada ya Bayern Munich.
Timu zote zinakabiliwa na baadhi ya majeruhi lakini asilimia kubwa ya wachezaji walio cheza mchezo wa awamu ya kwanza wapo fiti isipo kuwa Pirlo ambae ni majeruhi na nafasi yake itachukuliwa na Marchisio atakae saidiana na Pogba pamoja na Vidal huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Morata alie katika kiwango bora kwa kushirikiana na Tevez.
Aubameyang,Reus wataongoza safu ya ushambuliaji ya Dortmund huku Gundogan na Bender wakisimama kwenye dimba wakimkosa Sahin.
Vita kubwa itakuwa kati ya Gundogan na Vidal ambao ni miongoni mwa viungo bora kwa sasa, Dortmund ni timu inayo cheza kwa kasi sana lakini upande wa safu ya ulinzi imekuwa si nzuri tofauti na Juve timu iliyo kamilika kila idara.
Dortmund wamepoteza mara tano na kushinda mara tano walizo kutana na Juventus.
--------
BARCELONA vs MAN CITY
2 - 1
Pale Camp Nou vinara wa La Liga Barcelona watacheza dhidi ya Man City ambayo haina matokeo mazuri kwa hivi sasa huku kibarua cha kocha wake Pellegrin kikiwa mashakani.
Busquets hatokuwepo hivyo Mascherano atacheza kama kiungo cha chini na Mathieu atasimama beki ya kati na Pique.
Upande wa City Yahaya Toure atarejea kikosini baada ya kukosa mchezo wa kwanza huku Clichy akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyo oneshwa mchezo wa awamu ya kwanza.
Pengine Pellegrin akitumia 4-2-3-1 huku viungo wa chini wakiwa Toure na Fernando itawasaidia kupunguza makali ya Barca ambao stahili yao ni ileile ya kuuchezea mpira sana na mashambulizi ya muda wote.
Wamekutana mara tatu mpaka sasa ktk Uefa huku mara zote kukiwa na kadi nyekundu tatu kwa upande wa City ( Demichelis-Zabaleta-Clichy). Barca wakishinda mara zote na makosa ya ukabaji mbaya wa City ndo huwa yanawaponza pengine leo wasipo kuwa makini tutashuhudia kadi nyingine nyekundu.
Tangu 1992 ni mwaka 2007 timu kutoka England kupata ushindi Camp nou nao ni Liverpool kwa ushindi wa 2-1.
City wameshinda mara 1 2011 dhidi ya timu za Hispain baada ya kuwafunga Villareal 3-0 hivyo haitakuwa kazi rahisi kwa wao kushinda Camp nou.
Messi amefunga magoli 39 kati ya mechi 42 ndani ya Camp nou kwenye michuano ya Uefa na leo atakuwa miongoni mwa wachezaji wa Barca watakao kuwa na madhara mbele ya safu ya ulinzi ya Man City huku akiwa na kumbukumbu ya kukosa penalti kwenye mchezo wa awamu ya kwanza.
Aguero ni miongoni mwa wachezaji wasumbufu na wenye kuzifuma nyavu na leo Barca wasipo kuwa makini nae hasa kwa mashambulizi ya kushtukiza ya City tutahesabu mengine. Na huenda akaanza na Bony kutokana na kasi na nguvu alizo nazo tofauti na Dzeko.
TIMU ZILIZO FUDHU ROBO FAINALI MPAKA SASA:-
Real Madrid- Hispania
A.Mandrid-Hispania
Psg-Ufaransa
Monaco-Ufaransa
B.munich-Ujerumani
Fc Porto-Ureno
For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com
0 comments:
Post a Comment