ARSENAL vs W.HAM
Baada ya kutinga nusu fainal ya FA na kuwa nafasi ya tatu katika ligi nyuma ya pointi sita dhidi ya Man City walio nafasi ya pili. Arsenal watawakabili vijana wa Big Sam London derby pale Emirates.
Arsenal licha ya kuwa na majeruhi wengi hasa eneo la kiungo bado wanacheza vyema hasa kwa Coquelin na Cazorla kiwango bora walicho onesha katika mchezo wa FA dhidi Man Utd kitakuwa chachu ya kutafuta ushindi leo dhidi ya W.ham ambayo kwa hivi sasa hawana matokeo mazuri.
Chamberlain baada ya kuumia nyuma ya goti ktk mchezo dhidi ya Man Utd atakuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Arsenal watakao ukosa mchezo huu,hivyo Ramsey au Walcot watachukua nafasi kuungana kina Sanchez. Nguvu alizo kuwa nazo uwezo mzuri wa kukaba na umbile lake tutaraji kumuona Welbeck akianza kutokana na uwezo alio onesha dhidi ya Man utd pia na aina ya timu watakayo cheza nayo.
Katika michezo 11 wameshinda mchezo 1 huku pia kati ya michezo 13 hawajashinda mbele ya Arsenal wakitoa sare mbili na kupoteza 11 hawa ni W.ham tangu wafanye vyema mwezi wa 12 mwaka jana wamepotea timu imekosa ubunifu huku makosa ya kizembe ya safu ya ulinzi yaki wagharimu.
Watamkosa Valencia hivyo tegemezi litakuwa kwa Sakho pia tukitaraji kiungo cha kati kitaongozwa na Noble pamoja na Song anaerejea Emirates.
-----------
W.BROM vs STOKE CITY
Kipute kingine ni pale dimba la Haco thorns W.Brom watakapo wakaribisha Stoke City iliochini ya Mark Hughes.
Utamu wa mchezo huu ni kocha wa W.Brom ambaye amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi wa pili atakapo kutana na timu yake ya zamani.
Licha ya kutolewa katika robo fainal ya FA na Aston Villa,W.Brom wamehimalika sana tangu kutua kwa Pulis safu ya ulinzi imekuwa nzuri na katika michezo sita ya ligi mechi za nyumbani hawajaruhusu wavu wao kuguswa ktk michezo mitano.
Wapo nafasi ya 13 kwa pointi 30 bado wataendelea kumkosa Anichebe na Mcmanaman, Berahino akiwa ktk kiwango bora kabisa anataraji kuongoza safu ya ushambuliaji.
Stoke City wapo nafasi ya 8 wakiwa na pointi 42 wana historia nzuri pindi wakikutana na West Brom kwani katika michezo 11 wameshinda mara 7 na kupoteza mchezo 1.
Kwenye michezo hiyo 11 hawajaruhusu goli kwenye michezo nane dhidi ya W.Brom, Diouf,Moses na Crouch wanataraji ongoza mashambulizi huku Shawcross na Ireland wakirejea.
Mipira mirefu na mashambulizi ya kushtukiza ndo mbinu anayotumia Hughes mara nyingi.
Ngoja tusubiri ni kisasi cha Pulis au ni mwendelezo wa matokeo bora ya Hughes.
For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com
0 comments:
Post a Comment