Happy Birthday Mwalimu wa Waalimu
mnamo tarehe 21 ya mwezi wa 3 mwaka 1980
huko Port Alegre nchini Brazil, alizaliwa
mfalme wa Soka.
Ujio wake ulitarajiwa, kwani ishara nyingi
zilishajionesha kuwa mbarikiwa atakaekuja
kutambulisha skills zinazopatikana katika ligi
yu karibu kuzaliwa.
kuzaliwa na kukua kwake kulikuwa ni kwa
kibinaadamu zaidi na alisoma na kupata malezi
kama watoto wengine mpaka alipotimiza miaka
13 ndipo matendo ya kinabii yakaanza kuonekana.
Akiwa na umri huo Dinho aliisaidia timu yake
ya mtaa kupata ushindi wa goli 23-0 magoli
ambayo yote aliyatupia yeye.
Huyu ndiye Ronaldo de Assis Moreirra
almaarufu kama Ronaldinho Gaucho-The saint
ambae akiwa uwanjani basi Malaika huacha
shughuli zao na kuanza kumtazama.
Alipofika ulaya alitua katika timu ya Paris Saint
German ya huko Ufaransa ambapo matendo ya kimiujiza awapo uwanjani yalizivutia klabu nyiingi sana barani humo.
Nilikuwa niko darasa la 3 huko Ukonga-DSM,nakumbuka zilikuwa ni fainali za Kombe la dunia mwaka 2002 zilipigwa huko Korea Kusini na Japan.
Sikukosa mechi hata moja ambayo Brazil walikuwa wanacheza.Kwani sikupenda kukosa kuiona miujiza ya Ronaldinho Gaucho.
Huyu ndiye Gaucho aliyemfanya Kocha wa Brazil enzi hizo Luis Philipe Scoral amteme Gwiji wa soka wa Brazil wakati huo Romario kwa utovu wa Nidhamu,dunia nzima,waBrazil hadi rais wa Brazil alimshangaa kwa kumtema Romario.
Lakini Scorali alikuja kuibuka na kijana kutoka PSG Ronaldinho Gaucho na kufanikiwa kulichukua kombe hilo huku Goli la maajabu zaidi linakumbukwa ni lile la Robo fainali baina ya Brazil dhidi ya Uingereza,Dinho alipiga faulo ya ajabu iliyomshinda David Siemen na kujaa wavuni.
Hakudumu sana na PSG kwani Klabu za Manchester United na Barcelona zilimuwinda kwa udi na uvumba.
Lakini Barcelona ndio walikuwa katika mipango ya kuijenga timu yao.Pesa walikuwa nayo, uwanja walikuwa nao, ila kuna kitu wakawa wamekosa.Na hapa sasa ndipo ikawalazimu wamchukue
mtu atakaekuja kufanikisha kuiunda na kuipa
mafanikio.
Na ndipo msemo wa ;DINHO MADE BARCA AND
BARCA MADE MESSI ulipotokea.Hatimae Dinho akatua Nou Camp nou na kuanza ujenzi wa timu.
Barca ikawa timu ya ushindani badala ya
ushiriki..
Barcelona ikaanza kupata ushindi mfululizo katika mashindano yote, barca ikaanza kujaza uwanja kwani habari za miujiza ya soka anayofanya Saint Gaucho zilitapakaa ulimwenguni kote
mfalme Ronaldinho alitibu kiu za wote
waliokuwa na njaa ya kuuona ufundi wa mpira
Mfalme huyu hakujaliwa kukasirika kabisa.Anakupiga vyenga ukimkata anacheka tuuu.
Ronaldinho hakuleta mataji tu bali alijengea
heshima ambayo kamwe haiwezi futika
machoni mwa waliomuona ilifika hadi hatua
mashabiki kutoka timu yenye upinzani wa
damu na nyama na barca "real madrid' kiasi
cha kupewa standing ovation akiwa uwanja wa
santiago bernabeu.
kitu ambacho ni adimu kwa mchezaji wa barca kufanyiwa.Kama uliwahi guswa na miujiza ya "Ronaldinho Gaucho "tuungane kumtakia heri ya kuzaliwa na maisha marefu zaidi...
Wote tuseme Happy birthday "ronaldinho"
-katemi Methsela.
0 comments:
Post a Comment