Sunday, 1 March 2015
Uchambuzi wa mechi zote kali za leo ligi mbalimbali barani Ulaya na Mr.CHOI (KWA TAARIFA YAKO)
TOTTENHAM vs CHELSEA:- FAINAL Capital One Cup.
Mwaka 2008 katika fainali ya kikombe cha ligi tulishuhudia Jonathan Woodgate akifunga goli la kichwa katika muda wa nyongeza na kuipa ubingwa Spurs mbele ya Chelsea.
Vikosi vya timu hizo kipindi kile ilikuwa Robinson,Keane,Lediey King,Chimbonda,Zokola na Jenas hao ni baadhi wa Spurs huku kwa Chelsea ilikuwa kina Drogba,Anelka,Ballack,J cole,Belleti,Cech,Bridge na wenginewe lakini pia walikutana katika nusu fainal ya FA katika dimba hilo 2012 na Spurs wakapoteza.
Mara ya mwisho kukutana Chelsea walifungwa 5-3 katika mchezo wa ligi huku michezo miwili kabla ya huo Spurs walifungwa 3-0 kisha 4-0 Eden Hazard akifunga katika michezo yote hiyo.
Spurs wamekuwa hawana matokeo mazuri kwa kipindi hichi huku wakitolewa na Fiorentina katika Europa ligi licha ya kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji ikiongozwa na kinda Kane pamoja na Erikssen bado safu ya kiungo imekuwa haieleweki hasa kwa upande wa Dembele ambaye kiwango chake kimeshuka huku Mason akiwa katika kiwango kizuri.
Chelsea pigo kubwa kwao ni kumkosa kiungo bora kwa hivi sasa Matic ambaye amefungiwa mechi 3 kwa kadi nyekundu pengine tukamuona Mikel Obi aliye katika kiwango kibovu kutokana na ufinyu wa kupata nafasi ya kucheza au kati akasimama Ramires na Fabrepass, zaidi ya pengo hilo kikosi cha Chelsea hakitakuwa na mabadiliko sana zaidi ya Zouma na Cahil mmoja wapo anaweza kuanza huku Courtois akicheza kwa mara ya kwanza na jezi ya Chelsea pale Wembley.
Tangu Mourinho atue Chelsea kwa mara ya pili hii ndo fainal yake ya kwanza huku pia mpinzani wake pottetinho ikiwa fainal ya kwanza.
NB:: Tangu uwanja wa Wembley kufunguliwa upya Chelsea wamecheza mara 12 zaidi ya timu yoyote.
Chelsea wameshinda michezo 8 kati ya 12 waliocheza Wembley mpya.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
LIVERPOOL vs MAN CITY 15:00
Baada ya siku ya jana Southampton kupoteza mechi dhidi ya West Brom itakuwa nafasi kwa Liverpool wakishinda mchezo huu watafikisha alama 48 mpaka nafasi ya 4 wakisubiri matokeo ya Arsenal.
Rodgers ambaye timu yake imetolewa katika Europa ligi hii leo atamkosa Henderson aliye majeruhi huku Sakho ajulikan kama ataweza himili mikiki ya mchezo huu kutokana na majeraha yaliokuwa yanamsumbua.
Kwa upande wa Pellegrini baada ya kupoteza mbele ya Barca huku akiwa na nafasi ndogo sana ya kuendelea mbele katika michuano hiyo kombe pekee kwa City ni ligi kuu ndo wanaweza chukua,kikosi chake hana majeruhi huku Toure Yahaya akirejea baada ya kukosa mchezo dhidi ya Barca na ushindi wa leo utapunguza gepu mbele ya Chelsea hadi pointi 2 lakini Chelsea wanamchezo 1 wa kiporo kutokana na fainali ya Capital one wanaocheza leo.
Katika michezo 10 Liver hawajafungwa wakishinda mara 7 na sare 3 pia katika michezo 10 City kashinda mbele ya Liver michezo 3 katoa sare 6 na kupoteza 4.
NB:: Katika michezo 11 iliyofanyika Anfield City hajashinda mchezo hata mmoja huku akifungwa mara 7 na kutoa sare 4.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
ARSENAL vs EVERTON 17:00
Pale Emirates vijana wa Wenger baada kuchambangwa na Monaco watajiuliza mbele ya Everton timu pekee ya Epl kuingia 16 bora ya Europa ligi.
Katika Mchezo huu Arsenal wataitaji ushindi ilikurejea nafasi ya 3 huku Everton walio nafasi ya 14 ushindi kwao utawafanikisha kusogea hadi nafasi ya 12.
Majeruhi kwa vikosi vyote wapo wa siku zote nazungumzia upande wa Arsenal kina Ramsey,Arteta pia Oviedo,Mcgeady na Atsu kwa upande wa Everton.
Mchezo ni mgumu kwa pande zote kulingana na nafasi walizopo katika msimamo wa ligi kikubwa ni uwezo mkubwa wa Lukaku hivi sasa huku pia Cazorla katika ubora wake.
NB:: Katika michezo 20 kwenye michuano mbalimbali Arsenal wakiwa wenyeji Everton haija ibuka na ushindi huku wakipoteza 16 na sare 4.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
REAL MADRID vs VILLARREAL
Vinara wa La-Liga Real madrid walio na pointi 60 mbele ya Barca na A.Madrid watapambana na nyambizi wa manjano Villarreal walio nafasi ya 6 kwa pointi 44.
Vijana wa Marcelino Garcia mpaka sasa ndo timu ambayo haija ruhusu goli la kichwa watakuwa na kazi mbele ya Real Madrid ambapo Cristian Ronaldo mpaka sasa kashafunga magoli 5 ya kichwa.
Katika mchezo huu Real majeruhi ni walewale huku Nyambizi wakimkosa winga wa Urusi Denis Cherysher yeye ni mchezaji wa Real aliye kwa mkopo katika timu hiyo.
Kikubwa hasa katika mchezo huu tabkribani michezo 14.
Nyambizi hawajashinda pale Santiago wakitoa sare 3 na kufungwa michezo 11, huku Real wakihitaji ushindi kuongeza wigo wa pointi na Barca walio nafasi ya 2 hadi kufikia pointi 4.
NB:: Mpaka sasa Real ndo timu pekee ambayo haija toa sare katika michezo ya ligi wakishinda michezo 20 na kufungwa 4.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
SEVILLA vs ATLETICO MADRID
Pale Roman Sanchez Pizjuan vijana wa Unai Enery walio nafasi ya 5 kwa pointi 45 watacheza dhidi ya A.Madrid walio nafasi ya 2 kwa pointi 53 katika msimamo wa ligi.
Kikosi cha Sevilla kilicho ingia hatua ya 16 bora Europa ligi hakita kuwa na mabadiliko katika mchezo wa leo huku wapinzani wao wakimkosa Saul na Koke bado hajawa vizuri.
NB:: Katika michezo 10 iliyopita Sevilla hajashinda mbele ya vijana wa Simeone Atletico Madrid.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
PSV vs AJAX AMSTERDAM
Katika ligi kuu nchini Uholanzi-Eredivisie tutashuhudia mechi kubwa kabisa miongoni mwa mechi kadhaa barani Ulaya
Katika dimba la Phillips vijana wa Philip Cocu watapambana na vijana wa Frank de Boer Ajax ambayo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 50 nyuma ya vinara Psv walio na pointi 64.
Katika michezo 13 ya hivi karibuni Psv haijapoteza katika dimba lake la nyumbani huku katika mchezo huu wakiwakosa Schaars,Jozefzoon, pia Rekik na Arias hali zao hazija julikana.
Ajax watawakosa Fischer,Zimling,Sigthorsson na Klassen hali yake haijajulikana pia beki Joel Veitman akirejea.
Tutaraji mchezo wa kasi sana hasa kwa upande wa Ajax ambao pia wamekuwa na takwimu nzuri za kufunga nnje ya 18 tofauti na Psv.
Kulingana na msimamo ulivyo bado Psv ana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa hata kama watapoteza mchezo wa leo mbele ya Ajax.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
MONACO vs PARIS SAINT GERMAN
Tukihamia pale Ligue¹ ya Ufaransa katika dimba la Louis II Monaco walionafasi ya 5 na pointi 43 wata cheza dhidi ya Psg walio nafasi ya 2 kwa pointi 52.
Kikubwa hasa ni matokeo ya O.Lyonnais ambao walipoteza mbele ya Lille hapo jana hivyo Psg wakishinda mchezo huu watakwea kileleni kwa tofauti ya pointi 1 kwa Lyonnais wanapointi 54.
Katika michezo 5 timu hizi zilipo kutana kuanzia 18/12/2010 mpaka mwaka jana 5/10/214 matokeo yalikuwa ni sare, takribani michezo 4 ilikuwa sare ya 1-1 na sare nyingine ilikuwa 2-2.
Furaha ya Laurent Blanc ni urejeo wa Verratti na Luiz walio kuwa wamefungiwa huku mpinzani wake Leonardo Jardims kikosi chake kikiwa fiti kwa mchezo huo kikichagizwa na kiwango bora kwa hivi sasa cha Kondogbia,Corrusio,Berbatov na Moutinho.
NB:: Katika michezo 8 ya ligi iliyopita Monaco hawajafungwa.
______________________________________________
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa uchambuzi makini katika masuala mbalimbali hususan michezo.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Imeandaliwa na................
Mr CHOI
Choikangta.ckt@gmail.com
WhatsApp -0765 691418
0 comments:
Post a Comment