Kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ February 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni ishara kwa familia yake.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa Mheshimiwa John Komba ameongea na ripota wa BantuTz.com na kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia alianza kwa kusema "Taarifa
ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya wakati yupo njian
akawa anaweweseka sana,tulipofika TMJ hospital walipofanya vipimo
walisema ameshafariki’
Ripota:Kabla ya hapo kulikua na ripoti ya mzee kuugua?
Claudia John Komba:Zilikuwepo
baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika anajisikia
vibaya vibaya tukampeleka hospital ya Sanitas iliyopo Baraka Plaza,tukagundua
sukari imepanda sana na presha imepanda sana,akatolewa akawa anaendelea
vizuri,juzi tarhe 26 feb ilikua siku yangu ya Birthday’
‘Akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday
hii kwa sababu birthday nyingi huwa zinanioita nakua nipo nje kwa hiyo
birthday hii nataka nifanye kwa hiyo akatukusanya watoto wote,aliongea
maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke matabaka kwamba
huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na Mungu’.
0 comments:
Post a Comment