Facebook

Monday, 22 September 2014

Baraza laamuru mwili wa marehemu ufukuliwe Arusha.

Baraza la ardhi na nyumba mkoani
Arusha limeamuru mwili wa marehemu
Paulina Lucas aliyezikwa katika
eneo la mgogoro wa shamba katika
kijiji cha Elkiushin ufukuliwe mara
moja na kisha ukazikwe kwenye
makaburi ya umma .

Amri hiyo ilitolewa mwishoni mwa
wiki iliyopita na mwenyekiti wa
baraza hilo mkoani hapa ,Cyriacus
Kamugisha kufuatia shauri nambari
222 la mwaka 2006 lililofunguliwa
na Francis Levava aliyekuwa
akiwakislishwa na wakili,Ezra
Mwaluko.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo mbele ya
pande zote ,Kamugisha alisema kuwa
mnamo juni 11 mwaka 2006 mara baada
ya shauri hilo kufikishwa mbele ya
baraza hilo ilimariwa ya kwamba
kisifanyike kitu chochote katika
eneo hilo hadi shauri hilo la
msingi litakaposikilizwa lakini
upande wa wajibu maombi ulikiuka
agizo hilo.

Kamugisha,alisema kuwa upande wa
mlalamikiwa ambaye ni ,Kerusoi
Loilole aliyewakilishwa na wakili
Daud Haraka ulikiuka amri ya msingi
ya baraza hilo kwa kuzika mwili wa
marehemu sanjari na kujenga nyumba
na choo katika eneo hilo ihali eneo
lina mgogoro.
“Kitendo alichokifanya mjibu maombi
kuhifadhi mwili wa marehemu
hakikuwa sahihi kwani eneo lilikuwa
na mgogoro,kitendo hiki ni kudharau
amri halali ya mahakama”alisema
Kamugisha.

Hatahivyo,akisoma hukumu hiyo
mwenyekiti huyo alitamka kwamba
jengo la choo na nyumba
vilivyojenga katika eneo hilo
vibomolewe mara moja na kuagiza
zoezi hilo linapaswa kusimamiwa na
mkuu wa polisi wilayani Arusha(OCD)
pamoja na maafisa watendaji wa
kijiji na kata katika eneo la
mgogoro.

Alisema amri hiyo inapaswa
kutekelezwa mara moja kuanzia
tarehe ya hukumu na kimsingi maombi
ya mleta maombi yanakubaliwa kwa
gharama na baraza hilo kufukua
mwili wa marehemu huyo.
Akiongea mara baada ya hukumu hiyo
upande wa mlalamikiwa,Loilole
alisema kuwa hakumu hiyo haikutenda
haki na huenda ikazua maafa kwa
kuwa walianza kuzika miili
mbalimbali katika eneo hilo tangu
miaka ya nyuma hata kabla ya
marehemu Lucas.

Kwa upande wa walalamikaji kupitia
kwa wakili wake,Mwaluko alisema
kuwa wameridhishwa na hukumu hiyo
kwani imetenda haki kwani eneo hilo
ni mali halali ya mteja wake.

0 comments:

Post a Comment