Mafuriko yamewaua zaidi ya watu
200 nchini India na Pakistan huku watabiri wa hali ya hewa wakisema kuwa
mvua zaidi inatarajiwa kunyesha.
Majeshi ya mataifa yote mawili yanaongoza shughuli za uokoaji kwa kutumia ndege ili kujaribu kuyafikia maeneo ya vijijini.Takriban watu 100 wamefariki katika eneo la kashmir linalosimamiwa na India baada ya mafuriko hayo kuyasomba makaazi mbali na kusababisha maporomoko.
Maafisa katika eneo la kashmir linalosimamiwa na Pakistan wamesema kuwa takriban watu 110 waliuawa.
Ni mafuriko mabaya kutokea katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka sitini baada ya kuwashangaza raia waliodhani kwamba msimu wa kila mwaka wa upepo mkali ulikuwa umekwisha.
0 comments:
Post a Comment