Watu wengi wameripotiwa kufariki na wengine kujeruhiwa baada ya jengo kubwa la makao makuu ya Kanisa Kubwa la Mchungaji T.B Joshua lijulikanalo kama "Synagogue Church Of All Nations-SCOAN" ambalo liko chini ya Mchungaji na matabiri maarufu duniani T.B Joshua ambalo huwa linarusha vipindi vyake vya duniani kupitia kituo chake cha runinga kiitwacho TV Emmanuel.
Kanisa hilo liko katika eneo liitwalo Ikotum,Lagos-Nigeria.
Makao makuu ya kanisa hilo "SCOAN" inasemekana liliporomoka mida ya saa 12:45 hapo jana lakini hakuna chombo chochote cha habari kilichoruhusiwa kuripoti tukio hilo.Kuporomoka kwa jengo hilo kumesababisha vifo vya watu mbalimbali wakiwemo waumini kutoka mataifa mbalimbali.
Sehemu ya Ghorofa hilo iliyoanza kuporomoka ilikuwa ni kwa ajili ya wageni mbalimbali wanotoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kupata huduma za kiroho hususan maombezi na maajabu kutoka kwa mchungaji T.B Joshua.
BantuTz tumejaribu kufuatilia katika vyanzo mbalimbali kutafuta chanzo kilichosababisha kuanguka kwa Ghorofa hilo.
Na BantuTz tumebaini kuwa:Mwanzoni jengo hilo lilikuwa ni kwa ajili ya Ghorofa mbili pekee lakini baadae wakaongeza Ghorofa tano zaidi moja kwa moja unaweza ukagundua inawezekana jengo hilo lilizidiwa uzito.
Waliofunikwa na vifusi vya jengo hilo baada ya kuanguka ni pamoja na;wageni kutoka mataifa mbalimbali,baadhi ya wapishi,mafundi wa ujenzi wa jengo hilo,watumishi na waumini mbalimbali.
Magari mbalimbali ya kubeba wagonjwa yameonekana katika makao makuu ya SCOAN yakiwachukua majeruhi na miili ya watu waliofariki baada ya jengo hilo kuanguka na kuwapeleka katika hospitali ya Igando General na Isolo General
Baadhi ya wahanga hususan majeruhi wa tukio hilo wamekatiliwa kupokelewa katika baadhi ya hospitali za binafsi zilizo karibu na SCOAN kwa sababu ya kushindwa kumudu kuwahudumia wahanga wote wa tukio hilo kutokana na kuwa wengi sana
Baadhi ya wafanyakazi wa SCOAN walipokuwa wanahojiwa wamesema kuwa wahanga wengi wa tukio hilo ambao ni majeruhi wamekatika miguu na mikono.
Watu kutoka sehemu mbalimbali za Nigeria wamefurika katika makao makuu ya SCOAN waweze kuona kilichotokea hali iliyopelekea msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Baadhi ya askari Police wamekuwa wakali sana kwa waandishi wa habari ambao wanajaribu kutafuta kila njia ya kupata habari kuhusiana na tukio hilo,hali iliyopelekea wananchi kuhoji kwa nini askari Police wanawazuia waandishi wa habari kutoa taarifa kamili kuhusiana na hali halisi inayoendelea katika eneo hilo.mtafaruku mkubwa umeendelea hadi kufikia hatua askari hao kupiga risasi hewani kuwatuliza.
Mwandishi wa kituo Cha Runinga cha Nigeria "Nigeria Televison Authority-NTA" kamera yake imechukuliwa na askari Polisi.Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesikika wakizungumzia chanzo cha ajali hiyo sio jengo kuporomoka tu kwa sababu ya uzito lililokuwa nalo bali kuna sababu nyingine iliyosababisha kuanguka kwa jengo hilo.Huku wakisema jengo hilo lilianza kuanguka mara tu baada ya ndege iliyokuwa inazunguka juu ya jengo hilo kwa muda fulani kuondoka.
Lakini kiongozi wa Idara ya Ujenzi ya Mji wa Lagos,Bi.Abimbola Animashaun amesema hawezi kuthibitisha taarifa yoyote kuhusiana na kuanguka kwa jengo hadi hapo taarifa za uchunguzi wa kina zitakapokamilika.
Bi Abimbola alikaririwa akisema
"Tumekuwa hapa tukiwahoji kuhusu kibali cha ujenzi lakini hawajasema chochote kinachotushawishi.Wamesema wanakibali lakini hatuwezi kuthibitisha hilo.Tumewaambia watupe kibali cha ujenzi kinachotambuliwa na Serikali lakini hakuna yeyote aliyejitokeza kutoa kibali hicho"
Jana mida ya saa 12 za jioni katika Hospitali ya Isolo General wahanga 8 walikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Huku wengine 7 wakiwa katika uangalizi maalumu.
Inaaminika ni watu wengi wamepoteza maisha lakini kuna usiri mkubwa katika utoaji wa taarifa kwani mkuu wa Kitengo cha maafa Nigeria;Ibraham Farinloye alipopigiwa simu alisema ni watu 15 tu ndio waliopoteza maisha huku majeruhi wengi na miili ya watu waliofariki ikiwa katika hospitali karibia zote zilizo karibu na SCOAN katika viunga vya Jiji la Lagos hali iliyopelekea Hospitali za watu binafsi kukataa kupokea majeruhi na miili ya watu waliokufa kwa kushindwa kumudu idadi yao.
Lakini mkuu wa Police Kitengo cha Masuala ya Jamii jiji la Lagos,Ngozi Braide amekataaa kutoa idadi kamili ya majeruhi na idadi ya watu waliofariki katika ajali hiyo.
Kanisa hilo la maajabu "Synagogue Church Of All Nations-SCOAN" limejizolea umaarufu mkubwa duniani kote kutoka na maajabu,utabiri unaotimia,maono na tiba za kiroho wanaopokea watu wenye matatizo mbalimbali kutoka pande mbalimbali za dunia.
Gazeti moja kubwa na maarufu nchini Uingereza limeandika kuwa SCOAN linapokea wahudhuriaji wengi kuliko wale wanotembelea sehemu za kihistoria Uingereza kama vile Buckingham Place na "Tower of London"
Hadi BantuTz tunapomaliza kundaa taarifa hiiwatu wengi bado wamefukiwa katika kifusi cha jengo hilo huku pakiwa hakuna taarifa yoyote rasmi kuhusiana na kuporomoka kwa jengo hilo kutoka kwa Kiongozi na mwanzilishi wa SCOAN,Mchungaji,Mtabiri T.B Joshua
Sources:Vanguard.com/Nigeria
Imeandaliwa na............
{C.E.O BantuTz ENTERTAINMENT}
0 comments:
Post a Comment